2014-03-21 13:31:33

Kumbatieni ugonjwa na kifo mbele ya Yesu!


Ugonjwa na mateso yamekuwa daima kati ya matatizo mazito sana yanayoweka maisha ya mwanadamu katika majaribu. Katika ugonjwa mtu anapata mang'amuzi ya kutokuwa na uwezo, ya mipaka yake na kikomo chake. Kila ugonjwa unaweza kutufanya tuchugulie kifo.

Ugonjwa waweza kutupeleka kwenye uchungu, kujihangaisha wenyewe, pengine hata kukata tamaa na kumwasi Mungu. Waweza pia kumkoza mtu zaidi, kumsaidia kupambana katika maisha yake kile ambacho si cha lazima ili kuelekea kile kilicho cha lazima na muhimu katika maisha. Mara nyingi sana ugonjwa huchochea kumtafuta Mungu na kurudi kwake.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, ugonjwa na kifo si mwiko. Huu ni ukweli ambao watu wanapaswa kuukumbatia mbele ya Yesu.







All the contents on this site are copyrighted ©.