2014-03-20 14:42:25

Rais Filip Vujanovic akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 20 Machi 2014 amekutana na kuzungumza na Rais Filip Vujanovic kutoka Montenegro na baadaye alikutana pia na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na mgeni wake, kwa pamoja wameridhika kwa hali ya uhusiano kati ya Vatican na Montenegro pamoja na kuonesha nia ya kutaka kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Kanisa na Serikali kwa ajili ya mafao, ustawi na maendeleo ya wananchi wa Montenegro. Viongozi hao wamegusia pia masuala ya kimataifa na kikanda pamoja na kuangalia mchakato wa Montenegro katika harakati za kutaka kujiunga na taasisi za Jumuiya ya Ulaya.







All the contents on this site are copyrighted ©.