2014-03-20 15:08:14

Papa ahimiza watoto wote duniani kupanda mti na kuutunza kama ishara ya kutunza amani duniani.


(Vatican Radio) Papa Francisko Jumatano kama ishara ya kudumisha amani, alipanda mti halisi wa mzeituni, katika sehemu ya mpango wenye lengo la kuhimiza wa watoto wote duniani, kila mmoja, kupanda mti wake na kuutunza, kama kielelezo cha kuendeleza ufahamu juu ya amani na maana yake katika makazi yao , jamii, na nchi kwa ujumla. .

Papa alipanda mti wake kwa njia ya mtandao, akiwa katika makazi yake ya jengo la Mtakatifu Marta , wakati alipokutana na Wawakilishi wa Wasomi , kutoka mtandao wa Kidunia, unaounganisha shule pamoja ( “The Worldwide Network of Schools Getting Together”). Mpango huo huhamasishwa na Taasisi ya Kipapa ya Sayansi , ambacho Chansela wake ni Askofu Mkuu Marcelo Sanchez Sorondo wa Argentina.Papa , akihutubia kikundi cha wawakilishi wapatao 40,Papa alizungumzia juu ya umuhimu wa elimu, michezo na Mshikamano kuwa silha kuu katika ujenzi wa amani ya kudumu.

Kipapa Chuo cha Sayansi kinatoa mwaliko kwa shule zote kushiriki katika juhudi hizi katika ngazi zote za elimu, kama ilivyohimizwa pia na Papa Francisko, wakati akiadhimisha kutimia kwa mwaka mmoja, tangu aanze utume wake kama Papa, ambayo pia ilikuwa ni Siku Kuu ya Baba wote, na Siku Kuu Mtakatifu Yosefu. Papa aliitumia nafasi hiyo , kutoa mwaliko kwa shule zote kushiriki kwenye katika mpango huu katika ngazi zote. Na kupitia ukurasa wake wa Tweet , alipeleka salaam zake kwa shule zote kupitia mtandao wa Shule wa Dunia mtandao kwa Mkutano , ambamo alisema, leo tumepanda mti wetu wa mzeituni kwa ajili ya amani .









All the contents on this site are copyrighted ©.