2014-03-20 15:27:21

Kwaresima ni wakati wa kurekebisha tabia na maisha yako- Papa


Vatican Radio) Kwaresima ni wakati wa " kurekebisha maisha yako. Ni wakati wa kuwa karibu na Bwana . Ni ujumbe wa Papa Francis, mapema Jumanne, wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican. Papa alionya dhidi ya mawazo kujiona kuwa bora kuliko wengine . Na alikemea unafiki wa kujifanya wema na kumbe siyo. Tabia ya ubinafsi wa kujiona ni bora kuliko wengine, huo ni unafiki na ni kujidanganya mwenyewe, na ni ujinga wa kutoelewa kwamba, ni juhudi za mtu mwenyewe, zinazohitajika kuwa mtu wa haki.
Papa aliendelea kuelezea unafiki kwamba, ni yule anayetaka aonekane mtu mwema , mtakatifu, mwenye bidii ya kuiinua sala mbinguni na kuomba mbele ya macho ya wengine , kujiona kuwa ni wenye haki zaidi ya wengine, mtu mwenye kuwadharau wengine. Na mara nyingi wanafiki ni watu wenye majigambo ya kusema , Mimi Katoliki sana ,mjomba wangu alikuwa mtu mashuhuri , baba alikuwa mfadhili mkubwa wa Kanisa au familia yangu ilikuwa ni hodari katika sala, mimi nimesoma, mimi namjua Askofu, nafahamiana na watu wakumbwa wakubwa, Kardinali, Mapadre, mimi ni hivi ni vile nk lakini ndani ya mioyo yao hawana hata chepe ya upendo kwa watu wengine hasa watu wa kawaida. Mbele ya watu wa kawaida, hujitanua na hufurahia kujionyesha kama wao ni bora zaidi, na wenye kuwa na haki zaidi. Lakini kumbe , mbele ya bwana hakuna anayeweza kudai kuwa mwenyewe haki . Papa alisema, “Sisi sote tunahitaji kuwa waadilifu, wanyonyekevu na wapole, ili tupate mastahili ya kuonekana kuwa wenye haki mbele ya Kristu, ambaye ndiye mwenye haki pekee.
Kwa sababu hiyo , Papa alisema, ni lazima kuifuata njia ya Bwana, kwa unyenyekevu na sadaka ya majitoleo ,na si kuwa Wakristo wenye kujificha katika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Unafiki huo si Ukristu.
Hivyo inafaa kuhakikisha kwamba, Ukristo wetu si wa kinafiki lakini ni halisi. Ni halisi katika maana ya kukaa karibu na Bwana, kama ilivyokuwa katika somo la kwanza : "Jioshe mwenyewe na kuwa mtu safi, . Weka matendo yote maovu mbali na macho ya Bwana , acha kutenda mabaya na jifunze kutenda mema. Huu ndiyo mwaliko wa Kipindi cha Kwaresima.
Lakini , Papa Francisko pia alihoji kwa jinzi gani, tunaweza kutambua ishara za kuwa karibu na Kristu au kutembea katika njia zinazofaa nzuri?"
Ishara ya kuwa karibu au kukutana na Yesu Kristo huonekana katika kuwajali wengine wanaotuzunguka wake kwa waume, maskini na wagonjwa, kama Bwana anavyofundisha katika Injili ya Matayo sura ya 25.

Kwaresima ni kurekebisha maisha , ni kufanya mabadiliko katika maisha , ni kukubali kutekwa na Bwana na kukaa karibu naye. Ishara za kuwa mbali na Bwana ni unafiki, maana mnafiki , haoni haja ya kuwahudumia wahitaji walio karibu naye, ingawa kwa nje anaonekana kuwa mtu aliye katibu sana na kanisa, daima anaonekana kuwa mtu wa sala na mwenye imani. Ni mtu anayeridhika kuokolewa na mwenyewe – hivyo kujidanganya kuwa ni mtakatifu. Papa aliendelea kutaja ishara nyingine ya kwamba sisi ni tumevutwa karibu na Bwana ni kuwa watu wa toba na wenye kuomba msamaha , na wahudumu kwa ajili ya ndugu masikini .
Papa alisali ili Bwana atupe ujasiri wote na mwanga : mwanga kwa kujua nini kinatokea ndani mwetu , na ujasiri wa kubadilika, kuvutwa karibu na Bwana, maana ni vyema kuwa karibu na Bwana. "








All the contents on this site are copyrighted ©.