Papa awakabidhi wazazi, Mapadre na walimu wote chini ya ulinzi wa Mtakatifu Yosefu,
Mme wa Mama wa Yesu.
Umati mkubwa wa mahujaji na wageni wapatao 200 elfu,walifurika katika uwanja wa Kanisa
Kuu la Mtakatifu Petro, kusikiliza Katekesi ya Papa na kumpogenza kwa kutimiza mwaka
mmoja tangu anze utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Naye Baba Mtakatifu
Francisko licha ya sherehe hizo, pia alitoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni
kama kawaida ya kila Jumatano. Papa aliifungua Katekesi yake kwa kukumbusha kwamba,
tarehe 19 pia ni Siku Kuu ya Mtakatifu Yosefu, Mme wa Maria na Msimamizi wa Kanisa
la Ulimwengu. Na hivyo Papa aliitolea katekesi yake kwa ajili ya adhimisho la Siku
Kuu hii, akisema ni haki na wajibu kutoa shukrani zetu zote Mtakatifu Yosefu, kwake
kwa kazi ya kumtunza Mama Bikira Maria na mwanae Yesu. Na kwamba, fadhila na ulinzi
kwa familia, zilikuwa ni sifa za Mtakatifu Yosefu.
Papa aliendelea kusema
kwa Jumatano hii alipenda kuzungumzia mandhari ya Ulinzi wa mtazamo maalum wa elimu.
Kumtazama Yosefu kama mfano wa mwalimu ambaye anamlinda na kumsindikiza Yesu katika
njia yake ya makuzi kwa hekima, umri na neema, kama inavyo nena Injili ya Luka (
02:52 ). Papa alisisitiza hasa jinsi tunavyoweza kujaribu kutumia maneno haya tatu
- hekima, umri na neema - kama muhtasari kwa ajili ya kutafakari yetu.
Papa
alianza kufafanua juu ya umri , ambao zaidi ni asili ya maumbile kukua kimwili
na kisaikolojia. Yosefu na Maria walikuwa ni walezi wa kwanza wa Yesu katika umri
wake mdogo, kwanza zaidi ya yote walihakikisha kwamba yu salama na anapata mahitaji
yake yote muhimu, maendeleo ya kiafya. Na hatuwezi kusahau jinsi Yosefu alivyo hudumia
kwa uaminifu , hadi kuchukua jukumu la kukimbilia Misri kuyasalimisha maisha ya Yesu
dhidi ya ukali wa kitisho cha mauaji ya watoto kwa amri ya Herode. Na baada ya kurejea
tena nyumbani, katika makazi yao ya Nazareti , kwa muda mwingi , maisha ya Yesu ya
utotoni yalibaki siri ya ndani ya Familia Takatifu. Katika miaka hiyo Yosefu, alimfundisha
Yesu pia kazi yake, kama Yesu alivyoitwa kwa jina jingine Mwana wa Seremala (Mt 13:55)
.
Papa aliendelea kueleza juu ya mwelekeo wa pili wa elimu ya Yesu, yaani "hekima"
akirejea tamko la Maandiko Matakatifu, yanayosema kwamba: mwanzo wa hekima ni hofu
kwa Bwana ( angalia Mithali 01:07 ; Sir 1:14). Na alifafanua kwamba, hofu si kwa
maana ya woga, bali ya heshima takatifu, kuabudu , utii kwa mapenzi yake matakatifu,
ambayo daima yanaonyesha wema wetu. Yosefu alikuwa daima kwa Yesu mfano na
mwalimu wa hekima hii , ambayo ni hulishwa kwa neno la Mungu. Tunaweza kufikiri jinsi
Yosefu alivyomfundisha mtoto Yesu kusikiliza kwa makini Maandiko Matakatifu , na
siku ya Sabato aliandamana naye katika sinagogi la Nazareti . Na Yesu kusikiliza kwa
kina katika uhusiano wa binadamu na Mungu , uliwashangaza Yosefu na Maria, alivyo
weza kufafanua maandiko, na katika umri wa mdogo wa miaka kumi , alibaki katika hekalu
la Yerusalemu bila ya wao kujua , na baada ya siku tatu walimkuta , wakati wa kujadili
na walimu wa Sheria, ambao walishangaa katika hekima yake. Hapa Yesu ni umejaa hekima,
kwa sababu ni Mwana wa Mungu. Hata hivyo , Baba wa Mbinguni alimshirikisha Mtakatifu
Yosefu, mtoto Yesu aliweza kukua kwa hekima kamili" (Lk 2:40).
Na hatimaye
, Papa alikamilisha Katekesi kwa kueleza ukubwa wa neema aliyo kuwa nayo Yesu , akifanya
rejea katika Injili ya Luka ambamo mmeandikwa " neema ya Mungu ilikuwa juu yake"
( 2.40 ). Alisema, hapa hakika, umuhimu wa Mtakatifu Yosefu, unaonekana kuwa ni mdogo
zaidi katika mazingira ya umri na hekima. Lakini itakuwa kosa kubwa kufikiri kwamba,
baba na mama hawawezi kufanya kitu chochote katika kuelimisha watoto wao kukua katika
neema ya Mungu. Yosefu alifanya hivyo tena kwa kifani . Kwa kweli, alifahamu
kwamba, amemwoa mwanamke aliyejaa neema " (Lk 1:28) , na alijua kwamba Yesu alichukuliwa
mimba kwa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, katika uwanja huu wa neema , kazi ya Mtakatifu
Yosefu , zaidi ilihusika katika kusaidia utendaji wa Roho Mtakatifu katika mazingira
ya maisha ya Yesu, katika kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi na mkewe Mama Maria,
Mama wa Yesu. Na kwa mazingira hayo, elimu inakuwa zaidi sana kwa ajili ya imani ,
sala, kuabudu na kuyakubali mapenzi ya Mungu na mpango wake. Pia na hasa katika huu
mwelekeo wa neema , Yosefu, alimfundisha Yesu kwa misingi ya mifano ya maisha ya kuwa
mtu wa haki, " (Mt 1:19) ambamo daima ni kukubali kuongozwa na imani. Na yeye alijua
kwamba, wokovu hautokani na kuzishika sheria tu lakini kwa neema ya Mungu , upendo
wake na uaminifu wake.
Papa Francisko alieleza na kukamilisha mafundisho na
wito kwa wote, wake kwa waume kwamba, Utume wa Mtakatifu Yosefu, kwa hakika ni wa
kipekee na usioweza kurudiwa , kwa sababu Yesu ni wa kipekee. Hata hivyo, Mtakatifu
Yosefu anabaki kuwa ni mfano bora, hasa kwa akina baba katika mambo matatu kwa watoto
wao , kutoa elimu, hekima na neema kwa watoto. Papa amewakabidhi wazazi wote , mapadre,
na wale ambao wana jukumu la kutoa elimu katika Kanisa na katika jamii kwa ujumla,
chini ya Ulinzi wa Mtakatifu Yosefu. .