2014-03-19 14:23:58

Mwenge wa amani usaidie kudumisha amani rohoni!


Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, Mwenge wa Amani alioubariki baada ya Katekesi yake kwa Siku ya Jumatano tarehe 19 Machi 2014, utasaidia kuhamasisha upatikanaji wa amani ndani ya mioyo ya watu. Mwenge wa Amani ulipelekwa na wajumbe kutoka Shirika la Wabenediktini waliosindikizwa na waamini kutoka Norcia, Subiaco na Casino, nchini Italia.

Mwenge wa Amani utaanza kutembezwa kwenye baadhi ya Monasteri za Wabenediktini na baadaye utarudishwa kwenye miguu ya sanamu ya Mtakatifu Benedikto.







All the contents on this site are copyrighted ©.