Vatican Radio) Ili kupata huruma ni lazima kwanza ya kusamehe . Ni kwa njia ya msamaha
kwamba mioyo yetu , na dunia , hujazwa na amani . Ni maudhui ya Papa Francisko katika
homilia yake ya wakati wa Ibada ya Misa Jumatatu asubuhi, katika kanisa dogo la Mtakatifu
Marta la ndani ya Vatican.
Papa alieleza kwa kurejea maneno ya Yesu kwa wafuasi
wake aliposema, "Kuweni na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma" . Papa alionyesha
kutambua kwamba ,pengine siyo rahisi kuielewa hii tabia ya huruma kwa sababu tumezoea
kuhukumu. Na kwamba wengi tunakosa kuelewa maana ya huruma kwa kuwa hatuna asili hiyo
ya kusamehe.
Na ili kuwa na huruma, Papa aliendelea, kuna mambo mawili yanayohitajika.
Kwanza ni elimu ya mtu mwenyewe . Elimu hii binafsi ina maana ya kukiri kutenda
jambo baya ! Na hivyo kujiona ni mwenye dhambi, na hivyo kuiona haja ya kutubu na
kuiungamia haki ya Mungu, ambayo ina uwezo wa kumbadilisha mtu kwa huruma na msamaha
wake. Na hivyo, lazima tuone aibu kwa dhambi zetu na kuomba huruma ya Mungu
.
Papa aliendelea kufafanua kwamba “si lazima kutenda dhambi kubwa kama kuua
mtu , lakini kuna mambo mengi madogomadogo ambamo tunatenda dhambi, na dhambi ni
nyingi kila siku, na mtu anapaswa kuiona roho yake ni dogo kubeba dhambi zote na hivyo
anapaswa kuona aibu mbele za Bwana na mbele ya Mungu, na mbele ya wengine na hivyo
kuomba msamaha. Inaonekana kama ni rahisi, lakini ni vigumu sana kusema, Nimekosa”.
Papa
aliendelea kuonya kwamba, mara nyingi, ni vyepesi sana kuwalaumu wengine kwa ajili
ya dhambi zetu, kama alivyo walivyo fanya Adamu na Hawa. Ni rahisi kumsingizia mtu
mwingine, kwamba ndiye chanzo cha kutenda dhambi , lakini dhambi hiyo umeitenda mwenyewe!
Na iwapo tunapata utambuzi huo kwamba, tumetenda dhambi na kuomba msamaha kwa unyenyekevu
kwa sababu tunajisikia ndani mwetu kumkosea na tunahitaji huruma ya Mungu, vivyo
hivyo kama tunavyosali katika sala ya Baba Yetu : "Utusamehe , kama sisi tunavyo
samehe waliotukosea, ni lazima iwe hivyo, kuwa na huruma kwa wengine kabla hatujaomba
huruma ya Mungu kwa dhambi zetu.
Tabia nyingine tunahitaji kuwa nayo ili
kuipata huruma ya Mungu , Papa aliendelea, ni kuwa na moyo mpana, kwa sababu moyo
mdogo ni moyo wenye ubinafsi usio weza kuwa na huruma .
Moyo na huruma, alisema
Papa Francis, " hauna lawama , lakini husamehe na kusahau, kwa sababu Mungu husahau
dhambi zetu, Mungu hutusamehe dhambi zetu na hivyo moyo hupanuka. Hili ni jambo
nzuri , Papa alisema:” Wewe ni mwenye huruma " .
Watu wenye huruma, wanawake
kwa waume ni wale wenye mioyo mipana, ambao daima husamehe wengine na kufikiri juu
ya dhambi zao wenyewe. Hii ni njia ya huruma ambayo ni lazima kila mmoja aiombe.
Papa amesisitiza na kuhoji “kwa jinsi gani dunia ingekuwa ni dunia ya amani iwapo
watu wote, kama mtu binafsi, familia na vitongojini ,wangekuwa na tabia hii. Na
kwa jinsi gani amani ingekuwa mioyoni mwetu! Kwa sababu huruma huleta amani. Daima
tunapaswa kukumbuka :' Mimi ni nani kuhukumu ? Kuwa na aibu na kupanua moyo wako.
Bwana na atujalie neema hii