2014-03-18 08:57:23

Mtandao wa kidunia wa Wakatoliki, Waanglikana na Waislamu kukomesha utumwa mamboleo.



(Vatican Radio) Wawakilishi wa Wakatoliki, Waanglikani na Waislam, kwa mara ya kwanza, Jumatatu 17 March 2014, walikusanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Habari wa Vatican, kwa ajili ya uzinduzi wa Mtandao wa dunia Huru, wenye lengo la kukomesha utumwa mamboleo au biashara haramu ya binadamu, katika kipindi cha muongo huu.

Katika mkutano huo, Makubaliano msingi ya kufanya kazi kwa ushirikiano, jamii mbalimbali za imani, yalitiwa sahihi na Askofu Marcelo Sanchez Sorondo kwa niaba ya Papa Francis, ambaye pia ni Kansela Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Sayansi na Sayansi ya Jamii, ambayo imefanya utaratibu huu wa kuwakusanya pamoja watalaam mbalimbali ili kupata mtazamo wa pamoja katika kupambana na utumwa mamboleo, kufuatia semina ya Novemba mwaka jana. Pamoja naye pia alikuwepo Askofu Mkuu David Moxon , wa New Zealand ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kianglikani cha hapa Roma na mwakilishi wa Askofu Mkuu wa Canterbury kwa Baba Mtakatifu. Pia Makubaliano yametiwa saini na Dk Mahmoud Azab , anayemwakilisha Imamu Mkuu wa Al -Azhar, ambacho ni Chuo muhimu kwa dhehebu la Kiislam la Wasunni, ambacho kiko mjini Cairo Misri. Watu wengine muhimu walioweka saini katika hati hiyo ya makubaliano ni mfanyabiashara biashara mashuhuri Andrew Forrest , wa Australia, ambaye ni mwanzilishi wa shirika la Walk Free Foundation.
Waanzilishi wa Mtandao huu wa Dunia wanaamini, kwa kuhamasisha jamii kuu za imani duniani, itawezekana kuwa na matumaini mapya ya kufikisha mwisho utumwa mamboleo ifikapo mwaka 2020..
Wakatoliki, Waanglikana na Waislamu, wamezianza juhudi hizi na kile ambacho waandaaji wana matumaini kwa dhati kwamba, mtandao huu utaweza kupanuka na kupata wawakilishi kutoka jumuiya na imani zingine mbalimbali. Na wanatambua kwamba , mpaka sasa kazi kubwa tayari inafanywa kukabiliana na pia kusaidia upande wa mashtaka na ulinzi kwa waathirika . Lakini kinachokosekana mpaka sasa anasema Askofu Mkuu David Moxon Muanglikani , ni mbinu za pamoja kukabiliana na tatizo.
Amesema, ni kweli tu kwamba , kumekuwa na kazi zinazofanywa na Kanisa Katoliki , kanisa la kIaglikani na jumuiya zingine za kidini kwa kipindi cha miongo mitatu au minne kupambana dhidi ya biashara haramu ya binadamu lakini kilichokosekana ni ushirikiano wa pamoja. Na hivyo takwimu zinaonyesha pamoja na juhudi hizo, karibia milioni 30 wanaume , wanawake na watoto, waliingizwa katika utumwa mamboleo, na kwamba takwimu hizi ni nchi tu ya tabaka kubwa la barafu la watu wanaofanyishwa kazi kama watumwa.
Na hivyo waandaaji wanatumaini, juhudi hizi mpya za Mtandao wa Dunia huru, zitaweza kugusa mioyo ya waumini wote kusaidia kukomesha dhuluma hii, wanayoita ukiukwaji wa aibu wa utu wa binadamu







All the contents on this site are copyrighted ©.