2014-03-18 10:20:52

Matashi mema ya watu wa Argentina yawalishwa rasmi kwa Papa


Vatican Radio) Jumatatu Katika jengo la “Domus Santa Marta”, Papa Francisko alimpokea Rais Cristina Fernandez de Kirchner, Rais wa Jamhuri ya Argentina. Rais de Kirchner aliyekuwa amefuatana na ujumbe wake rasmi .

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Kiongozi huyo wa Argentina kukutana na Papa Francisko, kwa kuwa alikutana naye mara ya kwanza tarehe 18 Machi 2013, siku moja kabla Ibada ya Uzinduzi wa utume wake kama Papa. Na pia alikutana na Papa tarehe 28 Julai 2013, wakati wa Ibada ya Misa ya kuhitimisha Siku ya Vijana Duniani iliyofanyika Rio de Janeiro, Brazil.

Lengo la ziara ya Jumatat, ilikuwa kuwasilisha kwa Baba Mtakatifu Francisko, salamu na nia njema za watu wa Argentina, kwa ajili ya tukio la maadhimisho ya mwaka mmoja kupita tangu raia mwenzao wa Argentina, kuchaguliwa kuwa Papa .







All the contents on this site are copyrighted ©.