2014-03-17 11:47:59

Pascal Simbikangwa afungwa miaka 25 Jela kwa kosa la mauaji ya kimbari nchini Rwanda


Mahakama nchini Ufaransa imemtia hatiani Bwana Pascal Simbikangwa, aliyekuwa Kapteni wa Kikosi cha Ulinzi cha Rais wa Rwanda kwa kujihusisha na mauaji ya kimbari yaliyoitikisa Rwanda katika Mwaka 1994 kufungwa jela miaka 25. Kuanzia tarehe 6 Aprili a1994 hadi Julai 1994 zaidi ya watu millioni moja walipoteza maisha kutokana na mauaji ya kimbari.

Kapteini Simbikangwa amepatikana na hatia kwa kutoa silaha na habari kwa kikosi cha kijeshi kilichokuwa kinaendesha mauaji ya kimbari mjini Kigali dhidi ya Watutsi. Upande wa utetezi unasema kwamba, kesi hii inajikita zaidi katika ushahidi wa kisiasa.







All the contents on this site are copyrighted ©.