2014-03-17 10:49:28

Papa amewataka Wakristu vijana kutoona aibu kuwa Mkristo.


Papa Francisko, akiitembelea Parokia ya St Maria dell’Orazione, alikutana pia watoto na vijana wa Parokia hiyo, ambako aliwahimiza kuwa na ushujaa katika kuikiri imani yao na kutoionea aibu. Aliwahoji iwapo wanaona aibu kuikiri imani yao mbele ya wengine au kwenda kanisani. Aliwaambia kuna Roho Mtakatifu ambaye hutoa neema hii ya kutojisikia aibu kuwa Mkristo ! Na hii ni neema, kwa sababu, vinginevyo shetani daima hukaa kando tayari kutoa kishawishi cha kutokwenda Kanisani , akisema usiwe mjinga , ni wajinga tu ambao huenda kanisa . Shetani anachotaka ni uone aibu kuwa mfuasi wa Yesu.

Ili kujiepusha na nia hizo za shetani , Papa alisema ni lazima kuombe kwa Roho Mtakatifu, neema ya kutuondolea aibu hiyo. Papa alisisitiza hakuna aibu, kuwa mfuasi wa Yesu, kwani si ujinga wala si jambo la wazee, bali ni maandalizi ya kuupata uzima wa milele, ulioletwa na Yesu Mwenyewe kupitia njia ya kifo chake na Ufufuko wake.

Papa aliwahimiza vijana kumwomba Roho Mtakatifu, neema ya kutoonea aibu imani yao, huku akiwafundisha wanapokuwa mashakani, kuomba ujasiri wa kusema kwamba mimi ni Mkristo. Kuwa Mkristu asiyeonea aibu kuwa Mkristo, neema waliyo pokea wakati wa ubatizo.

Na pia , alizungumzia neno jingine lililotajwa katika Injili nalo ni hofu. Alieleza, Yesu alisema mara nyingi katika Injili, Msiwe na hofu. Lakini hofu hii inaendelea kuwepo kwa sababu shetani hujaribu kuijenga hofu hii hata ndani ya moyo ya waamini. Alitoa mfano wa kuwa na hofu ya kwenda katika Ibada ya Misa, hofu wa hiki na kile ... Lakini Mkristo anapaswa kuwa jasiri. Jasiri wa milele! Na ni vyema kufanya mambo, bila aibu au hofu ! Yesu aliwaambia mitume : Msiwe na hofu . Na hivyo Mkristu hapaswi kuwa hofu wala wasiwasi ..kwa sababu yu pamoja na Yesu, ambaye daima ni mlinzi na Mtetezi wa wetu. Na kamwe Yesu hautuachi peke yetu hata wakati wa majaribu na mambo magumu yu pamoja nasi. Na hivyo kama Wakristo hatupaswi kutenda dhambi kwa sababu ya hofu na wasiwasi. Tunapaswa kudumu katika kuomba kwa Yesu, neema ya ujasiri na kutokuwa hofu .

Papa alikamisha maelezo yake na sala kwa Roho Mtakatifu, ili awajalie wote ujasiri na kutokuwa na hofu katika kuitetea imani wakati wowote na katika hali zote, akiwataka wakati wote, wamwite Mama yetu Bikira Maria.








All the contents on this site are copyrighted ©.