2014-03-17 09:17:25

Kuisikiliza sauti ya Mungu kwa ajili ya kuilisha imani ni wito wa kwanza wa kila Mkristo- Papa


Jumapili iliyopita, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza Ibada ya Misa katika Kanisa la St Maria dell’ Orazione di Setteville di Guidonia , Parokia ya Jimbo la Roma, iliyo umbali wa kilomita ishirini, Kaskazini-Mashariki mwa Jiji la Roma. Hii ilikuwa ni ziara yake ya tano kutembelea Parokia za Jimbo lake , tangu aanze kuwa Papa.

Katika homilia yake alisisitiza kwamba, Kazi ya kwanza kwa kila Mkristo, kuboresha imani yake. Na kwamba kila Mkristu anapaswa kumsikiliza Yesu, kwa ajili ya kuiimarisha imani zaidi na zaidi, kuifanya imani kuwa na nguvu. Kwa kumwangalia Yesu , macho yetu huandaliwa na maono mazuri ya uso wake. Papa, alieleza kwa kuiangalia Injili ya siku ya Injili, ambayo ilieleza juu ya Yesu kubadilika sura yake. Papa aliwakumbusha waamini kwamba, Jambo la kwanza ni kubadilisha sura ya maisha.

Papa alieleza kwa kuuliza ni upi wajibu wa Mkristu? Je ni kwenda Misa Jumapili , kufunga na kujinyima wakati wa Wiki Mtakatifu; Yote hayo ni vyema... Lakini Kazi ya kwanza ya Mkristo ni kusikia Neno la Mungu , kumsikiliza Yesu, kwa sababu Yeye mwenyewe husema nasi, na Anatuokoa na neno lake. Kwa neno lake la nguvu, imani yetu huimarishwa na kuwa na nguvu zaidi. Ni kumsikiliza Yesu!

Papa aliendelea kurejea wale wenye kusema, lakini mimi namsikiliza sana Yesu, akihoji kwa vipi na wapi wanamsikiliza Yesu ? Je ni kwa kusikiliza tu redio, au kwa kusikiliza tu televisheni, au kwa kusikiliza tu porojo za watu mitaani juu ya Yesu. Papa aliasa kila siku tunasikiliza sauti nyingi nyingi. Lakini je tumewahi kutenga muda maalum kidogo tu kila siku kwa ajili hiyo? Kupata tu ukimwi wa kusikiliza na kutafakari neno la Yesu ulilolisikia na kujua maana yake nini katika maisha yako? Au tu ni basi ili mradi umesikiliza?

Papa aliwathibitishia wale waliokwa wakimsikiliza kwamba, Neno la Yesu lina nguvu zaidi kuliko chakula, kwa ajili ya roho , na kila siku huwasilishwa kwetu na Malaika wake , kama ilivyokuwa kwa mashahidi wa kwanza , kama alivyosema Mtakatifu Cecilia . Ni kila siku kusoma kifungu kutoka Injili na kuliruhusu neno hilo la Yesu kupenya ndani ya nyoyo zetu na kutupatia nguvu zaidi katika imani :

Papa amehimiza kila Mkristu inafaa kutembea na kitabu kidogo cha Injili mfukoni mwake , na wakati kunapokuwa na wakati, hata kama ni kidogo , mfano wakati wa kusafiri katika mabasi,tnapopata nafasi nzuri za kuketi kwa utulivu , kwa nini usisome Neno na kulitafakari. Injili daima i pamoja nasi.

Kisha Papa alizungumzia mambo mawili yaliyosikika katika Injili , sala na neema, ya utakaso wa macho, macho ya roho zetu, kwa ajili ya maandalizi ya uzima wa milele. Na kwamba Injili hii ya Yesu kubadilika Sura ni mwaliko wa kumsikiliza Yesu. Kubadilika sura Yesu kunatuonyesha Utukufu wake . Ni mwaliko na maono ya kutakasa macho yetu na kujiandaa kwa ajili ya uzima wa milele. Papa alionya pengine macho yetu, kidogo ni magonjwa au yamefunikwa na ukungu kwa sababu tunaona mambo mengi ambayo si ya Yesu, mambo yaliyo dhidi ya Yesu, mambo ya kidunia, mambo ambayo hayamulikii roho . Na hivyo mwanga wa Yesu tulioupokea, unasongwa na polepole kuanza kutoweka na giza kuanza kuingia ndani. Giza la kiroho, giza la imani : giza kwa sababu hatuna mazoea ya kuangalia, kufikiria mambo ya Yesu.

Kumsikiliza na kumtazama Yesu na mafundisho yake , ni wito kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Papa alihitimisha homilia yake akitoa wito wa kusoma Injili tena na tena na kuisikiliza sauti yake na kuona jinsi gani Yesu alifanya mambo. Na hivyo ndivyo akili na moyo huendelea kutembea katika njia ya matumaini.










All the contents on this site are copyrighted ©.