2014-03-17 12:32:45

Baba Mtakatifu akutana na wanajumuiya wa "Njia ya Ukatukumeni mpya".


Baba Mtakatifu Francisko, akikutana na wanajumuiya wa Ukatukumeni mpya,mapema mwezi uliopita mjini Vatican, alisema daima hufurahia kusikia mtu anatembea katika njia ya imani. Alieleza , maana yake, si kujifungia wala kusimama sehemu moja , bali ni kusonga mbele kwa bidii katika mwendo wa imani , kama ilivyo tokea kwa baba yetu Ibrahimu , ambaye aliisikia sauti ya Mungu ikimwambia toka, nenda ! Ni kutembea ! Kwenda mbele. Wapi? Mimi nitakuambia.
Papa alifafanua Ibraham, hakwenda kituo cha treni,au cha basi au kununua tiketi ya kwenda mahali fulani. Lakini alianza kutembea bila kujua wapi anakwenda, lakini akiwa na imani kwa Bwana! Hii ni moja ya sifa za Kikristo: kuwa njiani. Lakini si tu Mkristo , kila mtu waaminifu! Kwa kuwa mtu asiyekuwa katika njia ana kitu kinachomkwamisha kutembea pamoja na wengine nacho ni ubinafsi . Mtu anayeshindwa kusonga mbele katika mwendo wa maisha kwa kushirikiana na wengine au kujirudi makosa yake mwenyewe, mtu wa aina hiyo daima ana ubinafsi , na hawezi kutombea na wengine. Papa aliwatia moyo wanajumuiya, akiwakumbusha jinsi Abrahamu, baba yetu alivyoanza kujiandaa baada ya kuupokea wito wa Mungu, kujiandaa kutembea katika njia ya Yesu , ambaye Mungu alitaka kutuokoa sisi tulio katika mwendo wa maisha ya kiroho. Na kwamba, wakati wa Kwaresima sisi ni watu kutembea kuelekea Pasaka . Bwana hatuachi kamwe, daima anataka kuwa nasi katika njia hii ya wokovu wake. Daima ni kuwa juu ya njia ! Kwa sababu ni Mungu ambaye alifanya watu kutembea , alichagua watu na katika maisha yetu ya kiroho daima kusonga mbele, daima kutembea.

Pamoja na himizo hilo, Papa pia alitahadharisha juu ya hatari mbili na mitego ya njiani. Hatari ya kwanza, kama alivyoeleza Mtakatifu Teresa , ni mtu kuridhika na mahali alipofika na kusimama hapohapo. Papa alionya kwamba, huo ni upotofu kwa sababu mtu anatakiwa kuendelea na hija yake hadi mwisho wa maisha yake. Na ugumu wa pili ,kule kukosa kutembea katika njia ya haki: njia sahihi. Hii ni dhambi ! Kila mmoja anapaswa kutambua, kila tunapopotoka katika njia sahihi kwa kutenda dhambi , ni lazima kusahihisha na kisha kuomba msamaha kwa Bwana, kama kondoo waliopotea, na kuirudia njia ya Bwana, anayetuongoza na kutuwezesha wote kuendelea kutembea, katika njia sahihi.

Papa alikamilisha hotuba yake kwa kumwomba Bwana daima, na daima, tuwe njiani, kuianza historia ya wokovu, kama alivyofanya Baba yetu Ibrahimu, kuwa juu ya njia , tukiongozwa na kulindwa nae dhidi ya mitego mibaya inayoweza kuwa kikwazo katika kuendelea na hija hii hadi mwisho wa maisha yetu. Papa aliwashukuru wanajumuiya kwa uchaguzi wao wa kutembea katika njia hii ya Ukatukumeni mpya.








All the contents on this site are copyrighted ©.