2014-03-15 08:50:50

"Ut unum sint"


Ili wote wawe wamoja ndiyo kauli mbiu itakayoongoza hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Nchi Takatifu kuanzia tarehe 24 hadi 26 Mei, 2014, kama sehemu ya kumbu kumbu ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana, kusali na kuzungumza na Patriaki Anathergoras mjini Yerusalemu.

Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anatangaza hija hii alisema kwamba, hii ni hija ya sala itakayomwezesha kutembelea Yordan, Palestina na Israeli. Maeneo yaliyolengwa ni Amman, Bethlehemu na Yerusalem. Akiwa mjini Yersalemu, Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki Bartolomeo wa kwanza pamoja na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo nchi Takatifu watasali kwenye Kaburi Takatifu, ili kuombea umoja wa Kanisa. "Utu unum sint" Ndiyo Kauli mbiu inayoongoza hija ya Baba Mtakatifu Francisko huko katika Nchi Takatifu.

Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Francisko anakuwa ni Papa wa tatu kutembelea na kusali katika Nchi Takatifu. Wengine ni:
Papa Paulo VI aliyetembelea Nchi Takatifu kuanzia tarehe 4- 6 Januari 1964.
Mwenyeheri Yohane Paulo II alitembelea huko kuanzia tarehe 20- 26 Machi 2000.
Papa mstaafu Benedikto XVI alifanya hija ya kichungaji kuanzia tarehe 8 hadi 15 Mei 2009







All the contents on this site are copyrighted ©.