2014-03-14 15:10:15

Papa na wasaidizi wake warejea kutoka Mlimani kwa sala na mafungo!


Baba Mtakatifu Francisko amemshukuru Monsinyo Angelo de Donatis, Paroko wa Parokia ya Marko Mwinjili, Jimbo kuu la Roma, aliyeongoza mafungo ya kiroho kwa Papa pamoja na wasaidizi wake wa karibu. RealAudioMP3

Baba Mtakatifu anasema, mafungo haya yamekuwa ni msaada mkubwa katika hja ya maisha yao ya kiroho. Wamepewa mbegu ya Neno la Mungu itakayotunzwa na Yesu mwenyewe kwa kuipatia mvua ya kutosha hadi itakapozaa matunda yanayokusudiwa.

Baba Mtakatifu anasema, Padre De Donatis amekuwa ni nguri wa kupandikiza mbegu ya Neno la Mungu, kazi ambayo ameifanya kwa umakini mkubwa pamoja na kuhakikisha kwamba, lengo linafikiwa. Baba Mtakatifu anamwomba Monsinyo De Donatis kuwakumbuka na kuwaombea “viongozi na waamini hawa” ambao hata katika mapungufu yao ya kibinadamu bado wana ari na moyo mkuu wa kutaka kumfuasa Yesu Kristo kwa karibu zaidi, huku wakiwa na matumaini katika ahadi zake na kwa furaha zaidi.

Baba Mtakatifu tayari amekwisharejea mjini Vatican baada ya kwenda jangwani kwa takribani juma zima, tayari kuendelea na utume wake, akiwa amesheheni nguvu ya Roho Mtakatifu.








All the contents on this site are copyrighted ©.