2014-03-10 10:33:44

SECAM inaendesha Warsha kwa Makaribu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM, kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 14 Machi 2014 linafanya Warsha kwa ajili ya Makatibu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Kikanda na Kitaifa, huko Afrika ya Kusini.

Pamoja na mambo mengine Warsha hii inaangalia dhamana na wajibu wa Makatibu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki katika mchakato wa upatanisho, utawala bora, mafao ya wengi na kipindi cha mpito wa demokrasia Barani Afrika mintarafu Waraka wa Kichungaji, Dhamana ya Afrika, Africae Munus.

Makatibu wakuu wanatarajiwa kutayarisha Maadhimisho ya Mwaka wa Upatanisho Barani Afrika utakaofanyika kunako Mwaka 2015. Watashirikishana mang'amuzi na uzoefu mintarafu mada zinazofanyiwa kazi kwa sasa. SECAM inatarajia katika mkutano huu kuimarisha mikakati ya maendeleo ya SECAM tangu Mwaka 2013- 2016 pamoja na kuthamini mchango wa vyombo vya mawasiliano ya Jamii katika mchakato wa Uinjilishaji Mpya.

Ni mkutano ambao unawashirikisha viongozi mbali mbali wa Kanisa kutoka SECAM, Afrika ya Kusini na kwamba, Shirikisho la Maaskofu Katoliki Kusini mwa Afrika SACBC ndilo lililopewa dhamana ya kuratibu Warsha hii kwa Mwaka 2014.







All the contents on this site are copyrighted ©.