Kardinali James Francis Stafford, Mkuu mstaafu wa Idara ya Kipapa ya kitubio , ametoa
tafakari juu umuhimu na maana ya kupokea huruma ya Mungu wakati huu Mama Kanisa anapokianza
kipindi cha Kwaresima. Anasema, kipindi cha Kwaresima daima ni wakati ambamo Kanisa
zima: Wakatekumeni, na walimu wao, wadhamini, makatekista, Parokia - Kanisa zima,
hutafakari kwa makini huruma ya Mungu.
Amefafanua kwamba, huruma ya Mungu lazima
iwe hai katika maisha yetu binafsi kama Mkristo na pia maisha ya jamii zima ya waamini
wa Kristo. Ni wakati wa kuiishi huruma ya Mungu kimatendo, katika maana ya kusameheana
mmoja kwa mwingine. Kama Mkristu binafsi au jamii ya kanisa hailiishi hilo, basi
si wafuasi wa Yesu.