2014-03-07 11:16:05

Furaha ya kweli inabubujika kutoka kwa Kristo


Kipindi cha Kwaresima ni hija ya maisha ya kiroho ya siku arobaini inayowakumbusha Wakristo safari ya Waisraeli kutoka Utumwani Misri, wakatembelea Jangwani kwa miaka arobaini kabla ya kufika kwenye Nchi ya ahadi iliyojaa maziwa na asali. Wakristo wanakumbuka siku arobaini ambazo Yesu alikaa Jangwani akifunga na hatimaye akaribiwa na Ibilisi, kabla ya kuanza utume na maisha yake ya hadhara. Hizi ni siku arobaini za: kusali, kufunga, kutafakari na kutenda matendo ya huruma.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kwamba, furaha ya kweli inapata chimbuko lake kutoka kwa Kristo: mwaliko wa kukaa, kutembea pamoja na kuwa mfuasi wake mwaminifu.







All the contents on this site are copyrighted ©.