2014-03-07 12:50:12

Barua juu ya Ukusanyaji wa Sadaka, kwa ajili ya Nchi - Kardinali Sandri


Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki , Kardinali Sandri na Katibu wa Usharika Cyril Vasil, kwa pamoja wametoa barua yao walio ambatisha na nyaraka mbili: usambazaji wa mapato ya ukusanyaji mwaka 2013 na " Ripoti ya ulinzi wa Usimamizi wa Rasilimali Ardhi Takatifu katika Maeneo Mtakatifu 2012/2013 .


Katika barua yao wameeleza kuwa Kwaresima, ambayo ni kipindi cha kutembea pamoja na Kristo kwa msalaba na ufufuko wake, huamsha hisia zaidi za moyo wa udugu na wale ambao wanaishi katika Maeneo Mtakatifu. Mahali ambapo, mitume waliisikia sauti ya kwanza ya Bwana Yesu, pamoja siri za neema, na kisha kuwa kutangaza na kuwa mashahidi wa Injili ya Kristo. Katika mazingira hayo, Ukristu ulistawi na kupanuka tangu mwanzo wake katika mji kuanzia Yerusalemu.

Barua inaendelea kusema ,Umoja katika Kristo Mkombozi unawahimiza kwa mara ingine mwaka huu, kuona umuhimu wa kukuza mpango muhimu ya Makusanyo ya sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu “Collecta Pro Terra Sancta” , kutimiza ahadi ya kanisa la Ulimwengu , Mama Kanisa. Papa Francisko, alithibitisha umoja huo, wakati, akizungumza na Mapatriaki, maaskofu wakuu kuu Makardinali na Maaskofu, walipokuwa wakishiriki katika Mkutano wa Kipindi cha kwanza cha Mwaka kwa ajili ya Usharika kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki ambamo Papa aliyaelekeza Mawazo yake hasa katika Nchi Takatifu , ambapo Kristo aliishi, alikufa na kufufuka tena.

Na mpaka Usharika huo bado unazisikia sauti zilizotolewa na Mapatriaki, katika mwanga wa imani, ulio hai kweli. Mwanga wa Mashariki, unao aangazia Kanisa zima, tangu ulipojichomoza na kupanda juu kama mwanga wetu (Luka 1:78 ) , Yesu Kristo Bwana wetu, kama ilivyoelezwa pia katika barua ya Kitume ya “Mwanga wa Mashariki” (Orientale Lumen 1).

Na hivyo kila Kanisa Katoliki linapaswa kujisikia kuwa na deni la shukrani kwa makanisa yanayo ishi katika mkoa huo. Kutoka kwao, tunaweza, miongoni mwa mambo mengine , kujifunza kwa bidii mazoezi ya kila siku ya roho ya kiekumeni na mazungumzo. Kijiografia, kihistoria na kiutamaduni mazingira ambayo wao wamekuwa wakiishi kwa karne nyingi, kwa kweli , yanayo wafanya kuwa asili ya usharika wa madhehebu mengi ya Kikristo na dini nyingine.

Hata hii, makusanyo haya ya sadaka, yanakuwa ni chanzo kikuu cha riziki ya maisha na utendaji wa Wakristu hao Mashariki ya Kati. matendo yao, n akama yalivyo mapenzi ya Papa , yanayoomba sadaka ya Ijumaa Kuu, iwe ni kuonyesha kitendo cha mshikamano wa kweli na udugu wa karibu kwa Wakristu wa Mashariki.

Barua imetoa wito unaohimiza kuongozana Papa Francisko , anayejiandaa kuwa Hija ya amani na umoja katika Nchi Takatifu. Ziara inayo subiriwa kwa hamu na pia ni muhimu. Ziara inayo tazamiwa kuimarisha, kuwapa matumaini na kuwathibitisha katika imani ya Wakristo zaidi na zaidi kaika kuuona uwezo zaidi wa huruma , msamaha na upendo wa Mungu.

Baba Mtakatifu Francisko anatazamia kufanya ziara hii ya kitume Mei 24-26 2014, kutembelea Nchi Takatifu .









All the contents on this site are copyrighted ©.