2014-03-06 12:42:35

Kitabu na DVD: "Mwaka wa kwanza wa Upapa wa Francisko".


(Vatican Radio) Kituo cha Televisheni cha Vatican (CTV) kwa kushirikiana na Gazeti la kila wiki la Famiglia Cristiana , wametoa kitabu na DVD kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa utawala wa Papa Francisko. DVD hiyo, ina nakala za picha za baadhi ya matukio muhimu ya mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na ziara ya Papa Brazil na katika kisiwa Lampedusa Italia.

Na pia kuna dibaji za mikutano mbalimbali na umati wa watu waliokusanyika kwa wingi katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kuskiliza hotuba zake. Aidha baadhi ya nyaraka za awali zilizo chapishwa mara baada ya kuchaguliwa kwake kuwa Khalifa wa Mtume Petro. Na pia miondoko ya Papa inayoonyesha ishara na kudhihirisha jotojoto lake katika kulitumikia Kanisa la Ulimwengu. Msimulizi mkuu katika DVD hii ni muigizaji Italia Roberto Herlitzka, anayeonekana katika filamu mashuhuri iliyoshinda zawadi ya Oscar, filamu yenye jina “Ukuu wa Uzuri”.

Jumanne miongoni mwa wale walio wasilisha juhudi hizi kwa wanahabari , alikuwa rais wa Baraza la Kipapa kwa Mawasiliano Jamii , Askofu Mkuu Claudio Celli , ambaye alizungumzia ya njinsi Papa Francisko, alivyogeuza ukurasa mpya katika mtazamo wa Kanisa Katoliki kwa vyombo vya habari.

Alikiri Papa Francisko kuwa na uwezo mkubwa katika mbinu za kuwasilisha matukio, akisema, kwa kumtazama tu , mtu unakuwa huna neno , ila kufurahia ishara na maneno yake mazuri. Ana uwezo wa kuonyesha tukio, kuwa si yeye tena Papa Francisko, lakini ni upendo wa Mungu kwa binadamu, huruma ya Mungu kwa binadamu.


Kardinali aliendelea kuzungumzia uwezo wa Papa Francisko katika kutoa fafanuzi juu ya Injili akisema, mafundisho yake daima huguza moyo wa binadamu , na hili ni jambo kubwa.
Kitabu hiki kilichoandikwa katika lugha ya Kiitalino, kina jina “ Papa Francisko : Kanisa la huruma ' na DVD yake ina jina: Francisko : mwaka ya kwanza wa Upapa. Na vinauzwa kwa bei ya € 12.90 pamoja na gazeti “Famiglia Cristiana e Credere”








All the contents on this site are copyrighted ©.