2014-03-05 11:30:03

Kikundi cha Boko Haram kinaendelea kusababisha maafa makubwa


Kampeni ya Serikali ya Nigeria dhidi ya Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram bado haijafua dafu kwani kila siku, Kaskazini mwa Nigeria kuna watu wasiokuwa na hatia wanaoendelea kupoteza maisha yao kutokana na mashambulizi haya. Mashambulizi yaliyofanya hivi karibuni mji Mafa yamesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baadhi ya wananchi walilazimika kukimbilia nchini Cameron kwa kuhofia usalama wa maisha yao.

Taarifa zinaonesha kwamba, Boko Haram inaendelea kufanya mashambulizi pia nchini Camerun, hali ambayo inasababisha wasi wasi mkubwa kwa wananchi walioko Kaskazini mwa Nigeria. Hali hii itasababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Umoja wa Mataifa unasema, katika kipindi cha mwaka mmoja, zaidi ya watu laki tatu wamelazimika kuyakimbia makazi yao, watu ambao kwa sasa wanategemea msaada kutoka Jumuiya ya Kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.