2014-03-03 15:43:22

Salini kwa ajili ya Miito –


Baba Mtakatifu Francisko, amehimiza Wakristu, waongeze bidii kuombea miito ili wapatikane makuhani na watawa walio iva kweli kiroho kwa ajili ya kumtumikia Bwana peke yake. Watumishi walio jinasua kweli kutoka ubatili wa ibada za sanamu na mamlaka na fedha . Papa alitoa himizo hilo wakati wa Ibada ya Misa, Jumatatu hii asubuhi , akiwa katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta.

Hotuba ya Papa ililenga katika Injili ya Siku, ambamo mtu tajiri anapiga magoti mbele ya Yesu na kuuliza nifanye nini ili niweze kuupata uzima wa milele. Papa alisema, . Mtu huyu alikuwa na hamu kubwa ya kusikia maneno ya Yesu. Inaonyesha alikuwa mtu mwema, kwa sababu tangu ujana wake alikuwa ametii amri. Pamoja na utajiri wake, aliona bado kuna kitu anachokihitaji , Roho Mtakatifu, alimwongoza kwa Yesu, kutaja kujua zaidi cha . Yesu alimwangalia kwa upendo na kumwambia , nenda kauze vyote ulivyo navyo na njoo ufuatane nami katika kuitangaza Injili. Lakini hiyo , aliposikia hayo, alishikwa huzuni moyoni mwake kuachana na mali yake haikuwa rahisi.

Papa alisema, “Moyo wa tajiri, ulihangaika ,kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa akimtaka awe karibu na Yesu na kumfuata,nae alikuwa na moyo kamili lakini ulioinamia mali, na akuwa na ujasiri wa kuviacha alivyo navyo. Hivyo akachagua fedha . Moyo uliojaa matamanio ya fedha ...ingawa hakuwa mwizi, laghai, wala mwenye kuvunja sheria na makosa mengine ya jinai. Alikuwa mtu mwema na mwaminifu. Lakini moyo wake alifungwa na mapenzi kwa mali, alikuwa amefungamana na fedha na hivyo hawakuwa na uhuru wa kuchagua. Alichagua fedha kuwa msingi wa maisha yake”.

Papa alieleza na kurejea kwa jinsi gani vijana wengi , husikia ndani ya mioyo yao wito kama huu wa kuwa karibu na Yesu wakiwa wamehamasika na bila ya aibu hupiga magoti mbele ya Yesu na kuonyesha hadarani imani yao katika Yesu Kristo na wakiwa wanaonyesha moyo wa kupenda kumfuata yeye , lakini kumbe ndani ya mioyo yao pia wamejaa matamanio mengine mengi yanayowapokonya ujasiri wa kumfuata , na hurudi nyuma , furaha hayo ikiishia kuwa huzuni kubwa.

Kwa ajili ya hili, Papa amehimiza maombi k wa ajili ya vijana hawa ili mioyo yao ijae tu mapenzi kwa Yesu na kuwa tupu kwa mambo mengine. Kuwa na maombi kwa ajili ya miito,. Tusali ili Bwana, aweza kuwa na watumishi wengi wa kutuma katika shamba lake. Kutuma Mapadre, kutuma , kutuma watawa ,kutuma makuhani kwa ajili ya kuzuia ibada za sanamu, ibada ya sanamu ya ubatili , ibada ya sanamu ya kiburi , ibada ya sanamu ya mabavu, ibada ya sanamu ya fedha . Ni lazima tuombe kwa ajili ya kuandaa mioyo ya kumfuata Yesu kwa karibu.

Papa alisema mtu huyu katika Injili , alikuwa ni mtu mzuri mno lakini alikosa ujasiri wa kuachana na mambo ya duni aili aipate furaha ya uzima wa milelle. Leo hii kuna vijana wa namna hiyo, tunaohitaji kuwaombea ili wajinasue na utajiri wa dunia na mambo yake, badala yake washibishwe na utajiri wa kuwa karibu na Yesu na kumfuata.








All the contents on this site are copyrighted ©.