2014-03-03 08:48:47

Papa aomba amani Ukraine katika udugu wa Kikristo


Vatican ) Papa Francis. Jumapili wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , alitolea sala kwa ajili ya taifa la Ukraine ambalo liko katika hali tete ya Kisiasa kutokana na malumbano makali ya kisiasa.


Baba Mtakatifu alionyesha matumaini yake kwamba maeneo yote ya nchi " watajitahidi kuvishinda vishawishi vya kutoelewana na kujenga pamoja mustakabali wa taifa .Papa pia alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mpango wowote ule unaolenga kufanikisha mazungumzo na maelewano katika taifa hilo.


Papa aliutoa wito huo kupitia umati mkubwa watu waliofika kusali pamoja sala ya Malaika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu .
Kabla ya sala hiyo, Papa tokea dirisha la chumba cheke cha kujisomea linalo tazamana na Uwanja wa Kanisa Kuu la Matakatifu Petro , pia alitoa mafundisho mafupi juu ya masomo ya Jumapili, ambamo alisisitiza haja ya imani katika Maongozi ya Mungu na pia alisisitiza kama Wakristo , tunapaswa kuwasaidia ndugu na dada zetu wahitaji .


Papa aliendelea kuangalisha katika jamii ya leo, ambapo watu wanaishi katika hali halisi ya umaskini na matatizo mengine mengi yanayowakabili kama matokeo ya mgogoro wa kiuchumi ambao una dhalilisha utu wao. Papa alisema kuwa katika nyakati kama hizi maneno ya Yesu inaweza kuonekana si muhimu. Lakini katika hali halisi, bayana ni Yeye, mwenye kuwa na uwezo wote wa kutukwamua iwapo tutachagua kumtumikia. Maneno yaliyosomwa katika liturujia ya Neno, yanatukumbusha kwamba, hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili : Mungu na mali. Kwa muda mrefu kama kila mmoja hujaribu kujikusanyia vyake mwenyewe na daima ni wachache wanaofanya hivyo kwa haki.


Baba Mtakatifu alisema kwamba moyo unao chukua na tamaa yake mwenyewe ni mtupu kwa sababu Yesu alituonya juu ya utuajiri wa kweli ni utajiri wa roho, utajiri w a imani na si utajiri, wa vitu ambavyo baada ya kifo tunaviacha hapa , huliwa na mende na kutu na kuishia.


Paapa alibainisha kuwa Ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu inakosa mahitaji msingi, chakula, maji , mavazi, nyumba , kazi , afya, sisi lazima wote kutambua kwamba sisi ni watoto wa Baba aliye mbinguni , na kisha ndugu na dada" na tunapaswa kutenda ipasavyo kama Wakristo.


Aidha katika wakati huo, Papa alikumbusha kwamba kuelekea mwanzo wa Kwaresima. Alitaja mwelekeo huu kuwa ni kitendo cha kuanza safari ya kuongoka , ili kukabiliana na maovu kwa silaha za sala, kufunga na huruma .Papa Francis alisisitiza kwamba ubinadamu unahitaji ya haki, maridhiano, na amani , na kinacho takiwa tu ni kumgeuka kwa Mungu .









All the contents on this site are copyrighted ©.