Kampala) Maaskofu Katoliki Uganda wameonyesha mshikamano wao na serikali katika sheria
inayozuia ushoga, na wameridhia kuwekwa kwa adhabu kali kwa wale wanaotaka kufanya
ushoga hadharani , kinyume na kanuni za jadi na mila katika taifa la Uganda Katibu
Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda, Mons. Yohana Mbatizaji Kauta, alitaja
msimamo wa Kanisa Katoliki juu ya swala la ushoga kwa shirika la habari la CNS Februari
26, kwamba majibu yao na Kanisa ni wazi kabisa, hawaungi mkono ushoga. Lakini tangu
mwanzo suala hili limejadiliwa wamekuwa wakipinga adhabu kali za kupita kiasi kwa
vitendo vya ushoga kama kifo au kifungo cha maisha . Maaskofu kwa uelewa wao kwamba
, hiki si kilema cha kuzaliwa nacho mtu bali ni kujiendekeza, adhabu za kifungo zinawe
kutolewe lakini katika maana yakusaidia mtu aondokane na tabia hiyo mbovu katika jamii.
Maaskofu wanaamini kuwa kwa neema na maongozi mapya, mashoga wanaweza kubadilika.
Maaskofu walijadili na kutoa tamko lao wakati wakiwa katika kipindi cha mafungo ya
kiroho ambamo pia waliombea upatikanaji wa sheria mpya katika hali ya maridhiano na
amani.
Sheria dhidi ya vitendo vya ushoga ilianza kutumika tarehe 24 Februari,
baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kutia saini hati ya sheria hiyo. Muswada
awali ulipendekeza adhabu ya kifo kwa kosa la ushoga, lakini sasa sheria inataja
au kifungo cha maisha jela kwa wanaobanika kufanya ushoga hadarani , badala ya mapendekezoya
awali ya kifungo cha miaka 14 jela.
Nchi za Magharibi wafadhili na makundi
ya haki za kimataifa wameiita sheria mpya kuwa matumizi mabaya ya haki za binadamu
na wanaomba ifutwe. Marekani, na mataifa mengine yanayofadhili Uganda yamesitisha
misaada yake hadi sheria hiyo itakayofutwa, Katibu wa Nchi wa Marekani John Kerry
ameeleza katika taarifa yake.