Kongamano la kimataifa kuhusu haki msingi za binadamu
Kanisa na Haki Msingi za Binadamu ndiyo kauli mbiu inayoongoza Kongamano la Kimataifa
lililoandaliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Watu wa Slovakia hapo tarehe
4 Machi 2014. Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la haki na amani anatarajiwa
kushiriki katika kongamano hili kwa kupembua kwa kina na mapana kuhusu: haki msingi,
utu na heshima ya binadamu mintarafu Mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Baraza
la Kipapa la haki na amani linasema kwamba, lengo la Kongamano hili ni kuhamasisha
ushiriki wa Kanisa mahalia katika mchakato wa kulinda na kutetea haki msingi, utu
na heshima ya binadamu. Kongamano hili linawashirikisha viongozi wa Kanisa na Serikali
kutoka Slovakia. Wajumbe watapata fursa ya kusikia kuhusu nyanyaso na madhulumu dhidi
ya Wakristo Barani Ulaya.
Wajumbe watagusia pia haki za mashoga pamoja na uhuru
wa kidini nchini Slovakia; hali halisi na changamoto zilizopoto.