Changamoto ya maisha na utume wa Papa Francisko kwa Kanisa la Amerika ya Kusini!
Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini, tarehe 25 Februari 2014, imeanza mkutano wake
wa Mwaka utakaohitimishwa hapo tarehe 28 Februari 2014 kwa kukutana na kuzungumza
na Baba Mtakatifu Francisko.
Mkutano huu unajadili pamoja na mambo mengine
umuhimu wa Utume wa Papa Francisko kwa Kanisa la Amerika ya Kusini; hali ya maisha
ya vijana kutoka Amerika ya Kusini; uhusiano kati ya Vijana wa kizazi kipya na wanasiasa
pamoja na dhamana ya Kanisa katika malezi ya vijana wa kizazi kipya kwa kukazia haki
na amani. Wajumbe pia watapembua kwa kina na mapana Maadhimisho ya Siku ya Vijana
Duniani kwa Mwaka 2013 nchini Brazil.