2014-02-24 08:43:04

Ujumbe mzito umewasindikiza Makardinali wapya mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 23 Februari 2014 aliwashukuru wajumbe kutoka sehemu mbali mbali za dunia walioshiriki katika Ibada ya kuwasimika Makardinali wapya, jumamosi iliyopita pamoja na kuhudhuriwa Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Baadhi ya nchi kama Haiti na Brazil ziliwakilishwa na Marais wake. Ujumbe wa Burkina Faso uliongozwa na Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa; Ujumbe wa Canada uliongozwa na Waziri wa miundo mbinu. Kimsingi, nchi zilizotuma uwakilishi mzito ni pamoja na: Chile, Nicaragua, Ujerumani, Argentina, Corea, Jamhuri ya Wananchi wa Visiwa vya Dominican, Vietnam, Pwani ya Pembe, Hispania, Malta pamoja na Italia.







All the contents on this site are copyrighted ©.