Papa awahimiza viongozi wa kanisa kudumisha matumaini kwa watu wa Mungu
Jumapili 23 Februari, majira ya asubuhi , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa
Francisko aliongoza maadhimisho ya Ibada ya Misa akiwa na Makardinali wapya na Makardinali
wengine , kwa mujibu wa liturujia ya Jumapili ya V11 katika Kipindi cha kawaida. Ibada
iliyo hudhuriwa na maefu ya waamini waliofika kuwapongeza Makardinali wapya toka sehemu
mbalimbalimbali za dunia.
Katika homilia yake, Papa Francisko, aliitafakari
sala ya utangulizi ya Ibada :“ Baba Mwenye Huruma , kwa msaada wako , daima tuwe makini
kuisikia sauti ya Roho Mtakatifu" .
Papa alisema, Sala hii ya ufunguzi wa
Misa, inatukumbusha jambo msingi kwamba, ni wito wa kumsikiliza Roho Mtakatifu
ambaye hulichagamsha na kuliongoza Kanisa. Kwa nguvu yake ya ubunifu na upya , Roho
Mtakatifu daima hudumisha matumaini ya Watu wa Mungu, wanapo fanya hija katika njia
ya historia yao , na kama Msaidizi , yeye daima huwaimarisha Wakristu katika kuwa
mashaidi imara wa imani yao.
Papa alieleza na kusema wakati huo akiwa pamoja
na Makardinali Wapya, ulikuwa ni wakati wa kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu anaye
ongea nao kwa njia ya maandiko Matakatifu yaliyosomwa.
Papa baada ya kuyatafakari
masomo , aliwakumbusha Makardinali kwamba, Bwana Yesu na Mama Kanisa, wanatoa mwaliko
kwao, kushuhudia kwa bidii na hamasa zaidi katika nji hizi za utakatifu . Ni hasa
katika zawadi hii kubwa ya majitolea binafsi, yanayotolewa kwa uhuru kamili, ambamo
mna utakatifu wa kuwa Kardinali . Na kwamba kwa hadhi hii, wanapaswa kumpenda kila
mmoja, hata wale wanaonekana kuwa maadui kwao, wanaolenga kuwafanyia mabaya , kuwapinga
au kuwakaidi, wote ni kuwaslimia kwa tabasamu nzuri linalotokana ndani ya moyo wa
msamaha,huruma na upendo wa kweli, hata kwa wale wanao fikiri hawastahili. Ni hatua
ya kupinga kiburi kwa upole ; ni kuwa watu wa kusahau madharirisho na unyanyasaji
wanaoweza kukumbana nao. Daima ni kuruhusu kuongozwa na Roho wa Kristo, aliye jitoa
sadaka mwenyewe juu ya Msalaba, ili waweze kuwa njia kwa wengine pia , katika kuupata
upendo wake, na kuwa miongozi mwa wafuasi wake.
Papa ameitaja hii kuwa ndiyo
tabia ya Kardinali, ndiyo utendaji wa Kardinali. Kuitwa Kardinali katika Kanisa la
Roma la Ulimwengu , si kuingia katika mahakama ya kifalme, lakini ni kujiunga katika
huduma ya kina ya kusaidia wengine ili waepuke tabia mbovu na utendaji usiofaa unaochochewa
na fitina, uvumi, magenge ya uovu upendeleo au kupendelewa.
Papa alieleza
na kuomba lugha ya Makardinali na iwe lugha ya Injili, kusema ndiyo wakimaanisha kweli
ndiyo , na hapana iwe na maana ya kweli ya hapana , na miendo na fikira zao iwe katika
mtazamo wa Heri Takatifu kuwa njia yao utakatifu. Papa alikamilisha hotuba yake
kwa kuwasihi Makardinali wote kuwa wamoja katika Kristo na kati yao wenyewe kwa
wenyewe. Na aliwaomba wasimsahau katika sala zao , na pia ushauri na wamsaada wao
wa karibu katika kuliongoza Kansia la Ulimwengu. Vivyo hivyo alitoa mwaliko huo
kwa Maaskofu, Mapadre , Mashemasi, watawa wake kwa wanaume, na walei, akisihi kuisihi
pamoja na Roho Mtakatifu, na dekania ya Makardinali iweza daima kuwa na hamu zaidi
na hamu ya upendo wa kichungaji uliojaa utakatifu, kwa ajili ya kutumikia Injili
na kulisadia Kanisa kutoa miali ya mwanga wa Upendo wa Kristu katika dunia yetu.