2014-02-22 13:40:58

Papa awataja na kuwasimika Makardinali wapya.


Jumamosi hii majira ya saa tano, Papa ameongoza ibada hadhara ya Baraza la Makardinali ( consistori) ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutangaza na kuwasimika Makardinali wapya 19 aliowateua hivi karibuni.
Hotuba ya Papa, iliilenga katika Injili ya Mtakatifu Marko :10:32 , ambayo inasema "Yesu aliwatangulia mbele yao ".

Papa amesema hata kwa wakati huu , Yesu anatembea mbele yao, na daima atakuwa mbele yao. Ni yeye anayeifungua njia ya imani yao na furaha ya kuwa daima wafuasi wake , kukaa pamoja nae, na kutembea nyuma yake, kumfuata ..
.
Papa pia , aliirejea Ibada ya Misa ya mapema asubuhi, aliyo iadhimisha pamoja na Makardinali katika Kanisa dogo la la Sistine, la ndani ya Vatican, akisema, "kutembea" lilikuwa ni neno la kwanza lililopendekezwa na Bwana , kutembea na kisha kujenga na kuikiri imani. Na leo hii neno hilo linarejea tena, hatua inayo endelea hata sasa, Yesu anaendelea kutembea. Na hili ni muhimu . Yesu hakuja kufundisha filosofia au itikadi, lakini kuonyesha njia , njia ya kuandamana nae , njia ya kujifunza kufanya hivyo kwa kutembea pamoja nae..


Katika hotuba hii, Papa ameonyesha kutambua kwamba si rahisi , na pengine ni ngumu kwa sababu, njia aliyochagua Yesu , ni njia ya msalaba. Wakati akiwa njiani alizungumza na wanafunzi wake, nini kitatokea kwake akiwa Yerusalemu, ambako alitabiri mateso , kifo na ufufuko wake. . Wanafunzi walijawa na mshangao na hofu. Walishangaa, bila shaka, kwa sababu wao walidhani kwenda Yerusalemuni kushiriki katika ushindi wa Masihi, na kumbe ilikuwa tofauti, kama ilnavyoonekana katika ombi lililotolewa na Yakobo na Yohane. Wanafunzi walijawa na hofu ya kile kitakacho mtokea Yesu , pia ya wao kujiweka katika hatari ya kuteseka .

Na hivyo kumbe Papa aliwahimiza Makardinali wapy akwamba, wanapaswa kuwa tofauti na wanafunzi, maana kwa sasa wanafahamu dhahiri kwamba, Yesu ameshinda, na hivyo hakuna sababu ya kuhofia msalaba . Alisisitiza , ”kwa kweli ,matumaini yetu ni katika Msalaba . Ingawa bado ni binadamu na wenye dhambi, wakiwa mbele ya majaribu na fikira kama za watu wengine wa kawaida na si kama Mungu”
.
Papa aliendelea kuwaangalisha katika aya za Injili ya Marko 10:42, ambamo Yesu aliwaita wafuasi wake na kuwaambia nini maana ya kuwa mtumishi wa Mungu akisema anayetaka kuwa mkubwa kwenu , atakuwa mtumishi wa wote. Papa amesema hii ni ishara nyingine ya Bwana katika njia ya kumfuata
.
“ Ndugu zangu, Bwana Yesu anatuita mwenyewe! Kuwa pamoja naye na kumsikiliza , kupokea pamoja na kufurahia neno lake , kukubali kufundishwa na Roho Mtakatifu, na kuzidi kuwa zaidi ya moyo mmoja na roho moja , kuwa karibu na Yeye.

Papa pia amezungumzia umuhimu wa kushirikiana na wengine katika wito huu , kama hitaji muhimu kwa kanisa. Ushirikiano na Papa mwenyewe, na baina yao, kwa ajili ya kutangaza Injili Tukufu ya Yesu. “Kanisa linahitaji ujasiri wao wa kutangaza injili katika msimu na nje ya msimu, na kutoa ushahidi na ukweli. Kanisa linahitaji maombi yao, kwa njia sahihi katika kundi la Kristo. Na amewakumbusha Makardinali wasisahau kuomba na kulitangaza Neno la Injili kama kazi ya kwanza ya askofu. Pia Kanisa linahitaji huruma yao hasa wakati huu wa maumivu na mateso katika nchi nyingi duniani. Na , wajitahidi kuwa karibu kiroho na jumuiya ya kanisa na Wakristo wote ambao wanakabiliwa na mateso na ubaguzi.

"Ni lazima kukabiliana na mapambano dhidi ya aina zote za ubaguzi . Kanisa lina haja ya maombi kwa ajili ya wale wote wanaoteseka, ili wapate kuwa jasiri na imara katika imani, kujua jinsi ya kukabiliana na ubaya kwa wema. Na maombi yao yanahitajiwa na kila mtu , anaye teseka kwa sababu ya kudai haki ya uhuru wa imani ya kidini. "


Kanisa – pia alisema, lina haja ya kuhakikisha kwamba , Makardinali na viongozi wengine wa Kanisa ni watu wa amani na si imani ya maneno tu lakini matendo, kama hamu yao kubwa na nia ya sala zao. Kwa ajili hiyo , Papa alisutumia muda huo kuomba amani na maridhiano, kwa ajili ya watu wote ambao kwa waktai huu , wanapambana na ghasia za vita na wale ambao wametengwa na vita.


Papa alihitimisha hotuba yake kwa kuwashukuru ndugu zake katika Kristu, kwa kutembea pamoja nae nyuma ya Bwana, huku akiwasihi daima wauishi wito wao zaidi na zaidi, miongoni mwa kundi la waamini aminifu, watu aminifu kwa Mama Kanisa Takatifu








All the contents on this site are copyrighted ©.