Waziri mkuu mstaafu wa Italia anamshukuru Papa Francisko
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano jioni tarehe 19 Februari 2014 alifanya mazungumzo
ya faragha na aliyekuwa Waziri mkuu wa Italia Bwana Enrico Letta. Taarifa kutoka Ikulu
ya Italia inasema kwamba, mazungumzo haya yalikuwa ni ya maana sana.
Waziri
mkuu mstaafu Letta ameguswa sana na mazungumzo yake na Baba Mtakatifu Francisko na
amemshukuru na kwamba, ataendelea kutunza moyoni mwake mazungumzo haya hata kwa siku
za usoni! Bwana Letta ambaye anatoka Chama tawala cha PD, tarehe 14 Februari 2014
aliamua kung'atuka kutoka madarakani baada ya kushambuliwa na Chama chake kutokana
na kusua sua kufanya mabadiliko makubwa katika masuala ya kiuchumi. Matteo Renzi ndiye
aliyepewa dhamana ya kuunda Serikali Mpya ya Italia kwa sasa.