2014-02-21 09:37:45

Mchango wa Kardinali Walter Kasper katika Mkutano wa Consistori


(Vatican) Mkutano wa Maaalum wa Makardinali “Consistori”ulioanza mapema Alhamis katika ukumbi mpya wa Sinodi mjini Vatican , ulihudhuriwa karibia na Makardinali 150, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Vatican , Padre Federico Lombardi alipozungumza na wanahabari , juu ya maendeleo ya Kikao cha Consistori, kinacho lenga zaidi kuijadili mada ya familia.

Padre Lombardi akizungumza na wanahabari Alhamis mchana , alieleza kuwa baada hotuba ya Papa , Markadinali walituma salaam zao za upendo wa dhati kwa Askofu Mkuu Loris Capovilla , mmoja wa Makardinali mpya wanaotarajiwa kusimikwa na Papa siku ya Jumamosi katika kikao hiki, lakini kutokana na afya yake kutokuwa nzuri, hataweza kusafiri hadi Rome , lakini basi atakuwepo nao kiroho.

Padre Lombardi aliendelea kueleza kwamba, katika kikao hiki cha kwanza kwa mkutano huu , utangulizi wa Mkutano uliwasilishwa na Kardinali Walter Kasper. Lakini hati ya hotuba yake haitkuolewa hadharani kwa kuwa, inakusudiwa kutumiwa tu na washiriki wa mkutano na si vinginevyo. Na wajumbe waliutumia muda mwingi kusoma yaliyomo katika hati hiyo, na baadaye kuijadili na kutoa maoni yao .
Padre Federico Lombardi ameeleza kuwa, yaliyoandikwa katika hati hiyo yanaoana na hotuba ya Papa Francisco, juu ya uhalisia na kina cha familia, kwamba ,ni familia inaonekana kuwa jambo jema sana , lenye kuwa na utajiri mwingi wa matumaini na furaha lakini pia huishi na matatizo na vipingamizi kama sehemu ya maisha yake . Na kwamba suala zima la familia ni lazima kulitazama katika mtazamo chanya wa kugundua na kutangaza Injili ya familia kuwa mpango wa Mungu, na uzuri wake wote ,wenye kutoa kishawishi cha kweli katika mazuri yake yote, ya mke na mme kuungana na kuwa kitu kimoja kama familia.
Suala jingine muhimu lililotajwa katika hotuba ya Kardinali Kasper , ni dhana ya familia kama kanisa ndogo la nyumbani , na familia ndani ya Kanisa ambako hukutana na ukweli wenye kuionyesha njia yake ya kutemb ea kuelekea siku za baadaye, na jinsi familia inavyoweza kupata upendelea wa kuwa chombo cha uinjilishaji mpya. Kardinali Kasper amelizungumzia kanisa la nyumbani kwa mapana zaidi huku akifanya rejea si tu katika kiini cha familia lakini pia katika mpanuko wa jumuiya , vikundi vya kikanisa n,k.

Kwa maoni yake rasmi , Padre Federico Lombardi aliweka bayana kwamba, Hotuba ya Kardinali Kasper , haidai kuyataja mada zote zinazohusiana au kuhusiana na familia , wala haikujaribu kutoa utangulizi kwa yanayotarajiwa kujadiliwa katika sinodi ijayo, lakini ni kama ufunguzi rasmi wa Mada ya familia. Utangulizi wake ulielnga zaidi katika kuigundua Injili ya familia inayochupuka kutoka utaratibu wa Mpango wa Mungu katika uumbaji wa vitu vyote. Pili , ililenga katika mifumo ya dhambi ndani ya familia yenye kuzaa matatizo mivutano,na wasiwasi kati ya wanaume na wanawake, mwili na roho, kutengana na kutalakiana na mateso ya wanawake na mama , nk. Mwisho, ni kutafiti masuala ya familia katika taratibu za ukombozi , kwa kufanya rejea katika nyaraka za Injili na Agano Jipya kAtika masuala yanayohuisana na familia kama vile barua ya Mtume Paulo kwa Waefeso. Pia kuiheshimu ndoa kama Sakramenti, na neema yake ya kutakatifusha. . .

Aidha Kardinali Kasper pia alifanya rejea katika masuala ya waliotarakia kuoa tena akiifikiria ukina wa mfumo huu, unaotafuta kujipenyeza kama mtindo wa kufaa. Lakini amesema kwamba, eneo hili ni muhimu kujadiliwa pamoja , katika muono wa huduma za kichungaji, kwa misingi isiyoweza kutenganishwa na mafundisho sadikifu ya Imani na maneno ya Yesu Kristu , na uelewa wa huruma ya Mungu. Kardinali Water Kasper ameeleza na kurejea kazi Papa Mstaafu Benedict XVI , juu ya suala hili , ambamo yeye aliweka mkazo zaidi wa kuwa makini katika sakramenti ya kitubiokwamba, pengine inaweza kutoa njia ya kusaidia hali ngumu katika suala hili . Na pia aliikumbuka hotuba ya Papa Francisko kwa wafanyakazi wa Romana Rota mwanzoni mwa mwaka huu , amb amo alizungumzia juu yathamani ya ndoa ,akithibitisha kwamba hatua za kisheria si upinzani.

Fr. Lombardi alihitimisha muhtasari wake kwa wanahabari akisisitiza kwamba, Kardinali Walter , ametoa msisitizo mkubwa muhimu katika ukuu wa sheria za ndoa au tuseme maendeleo kuelekea aina mpya ya kuchunguza kwa kina siri ya ukombozi katika Kristo, kupitia uelewa wa ukweli wa sheria za injili.








All the contents on this site are copyrighted ©.