2014-02-21 10:46:14

Ili kumjua Yesu ni lazima kufuata nyayo zake ..


(Vatican) Kumjua Kristu ni kutembea nae katika utendaji wote wa kila siku na si kumfahamu kinadharia au kwa kusoma tu maandishi yake. Huo ulikuwa ni ujumbe wa Papa Francisko wakati wa Ibada ya Misa Alhamisi asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta. Alieleza kwamba , kila siku Kristu hutuuliza "Yeye ni nani kwetu" , na inawezekana tu kutoa jibu kwa kuishi naye kama iilivyokuwa kwa wanafunzi.

Papa amesema Ukristu ni maisha ya mwanafunzi , kuliko maisha ya utafiti. Mkristu kuujua ukweli wa Yesu ni nani kwake, ni kuingia katika hija na kufuata nyayo za Mwalimu wa ushuhuda wazi , na uvumilivu katika yote, usaliti , udhoofu wa mwili na kupita katika mashinikizo mapya yenye mikingamo mikali. Papa Francisko alieleza na kutoa mfano wa Petro , ambaye katika Injili ya siku ilimwonyesha yote kwa wakati mmoja, kama shahidi shupavu , anayejibu maswali ya Yesu kwa Mitume , “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani kwenu”? akijibu "Wewe ni Kristo" , na mara baadaye akawa kinyume chake, akamkana kama adui , na mara akipatwa na aibu , akaona anahitaji kukutana tena na Yesu, ambaye alikuwa tu ametangaz a mateso na kifo na ufufuko wake. Papa aliasa, mara nyingi ,Yesu anarudi kwetu na kutuuliza , “Mimi ni nani kwako” na tunampa jibu kama hilo la Petro, , Jibu tulilojifunza wakati wa Kateksimu , lakini jibu hilo halitoshi.

Papa aliendelea kufafanua kwamba, inaonekana kutoa jibu katika swali hilo tunaliliosikia ndani ya mioyo yetu , Yesu ni Nani kwatu, kwa yale ambayo tumeyasikia na kujifunza haitoshi. Wala kusoma na kuelewa peke yake haitoshi . Kumjua Yesu kweli , ni kutembea na Yesu katika njia yake, kama Mtume Petro alivyofanya ,baada ya kumkana, aliuona ukweli wa Yesu ni nani na kubadili mwenendeno wake . Petro alikwenda mbele na Yesu,alizona ishara alizofanya, aliona nguvu za Yesu, na kumkiri kuw andiye Kristu.

Petro , Papa Francisko aliendelea, aliomba msamaha kwa Yesu - na bado, baada ya ufufuo, aliulizwa na Yesu mara tatu katika mwambao wa ziwa Tiberia : " Wanipenda ?". Pengine, Papa alisema ,Yesu alitaka kuthibitisha upendo kamili wa Petro kwa Bwana wake , Petro alitokwa namachozi na kuona ea aibu wakati alipomkana mara tatu wakati wa mateso yake.

Papa anasema , ni kukutana kila siku na Bwana, kila siku ni kumshudia ushindi wetu na udhaifu wetu." Lakini , safari hii hatuwezi kuifanya wenyewe, tunamhitaji Roho Mtaktifu , aingilie kati , kama jambo muhimu.


Papa amehimiza, kumjua Yesu ni zawadi itokayo kwa Baba , ni Yeye anaye tufanikisha kumjua Yesu. Ni kazi ya Roho Mtakatifu, anaye fanya kazi hii kubwa. Hizi si kama juhudi za kibiashara au mashirikisho ya wafanyakazi , lakini ni Roho Mtakatifu, Mfanyakazi hodari ambaye daima huifanya kazi yake . Huifanya kazi hii ya kueleza fumbo la Yesu na kutupatia sisi maana ya Yesu ni nani kwetu. Papa aliomba tuyaweke mawazo yetu wakati ule wa Yesu akiwauliza mitume wake , Petro , Mitume ,tulisikie swali hilo a ndani ya mioyo yetu, “ Mimi ni nani kwako”? Na kama wafuasi wake na tumwomba Baba atujalie sisi sote, kumjua Kristo katika Roho Mtakatifu, ambaye atatupa jibu , la siri huu kuu , Yesu ni nai kwetu. .









All the contents on this site are copyrighted ©.