2014-02-20 11:04:14

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yazindua ombi dhidi ya unyanyasaji


Mkutano wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidi wazindua ombi dhidi ya unyanyasaji wa binadamu na tafakari: Je, dini zinaweza kukomesha unyanyasaji dhidi ya binadamu? Swali hilo limetolewa kwa viongozi wa dini zote, wakitakiwa kutoa kutoa jibu sahihi kwa mujibu wa imani yao.

Swali hilo ni hoja iliyojadiliwa katika mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu 'Egidio , kutazama mahusianao yaliyopo kati ya “Dini na Vurugu” , ambao ulihudhuriwa na wajumbebe kutoka dini kuu tatu, Wakristu , Wayahudi na Waislamu, pamoja na mabalozi , wasomi na wachambuzi wa mambo.

Sabatinelli wa Redio Vatican akitaarifu tokea mkutano huo ametaja kati ya waliohudhuria mkutano huu ni Kardinali Walter Kasper , Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Wakristu. Hotuba yake kwa mkutano huu ilileleza kwamba uhafidhini na ugaidi ni mambo yanayaweza kuchafua dini , na kuifanya dini kuwa tena si chombo cha kueneza amani bali vifo. Kardinali alieleza hayo akitazama baadhi ya migogoro iliyopo sasa sehemu mbalimbali za dunia , maeneo ya Afrika , Mashariki ya Kati , na Asia. Vurugu nyingi zinazofanywa kwa kisingizio cha kulinda haki za kidini kwa kutumia vurugu.

Kardinali Walter Kasper alisema, kama ilivyokwisha elezwa katika mikutano mingine ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio hapa Roma , licha ya tofauti za mafundisho na mapokeo ya kidini, ilithibitishwa kwamba, hakuna dini inayo halalisha vitendo vya unyanyasaji, vurugu na mauaji. Na jina la Mungu haliwezi kutumiwa kuhalalisha ugaidi. Na kwamba ni lazima na hawawezi kusahau kwamba, kuna watu wanaoteseka na kuathirika kwa sababu ya imani yao, wakiwemo Wakristo . Hivyo, kama viongozi wa kidini, hawawezi kukwepa uchunguzi wa dhamiri, na wajibu wa kukemea vikali utendaji wowote unaolenga kuvuruga mahusiano mazuri kati ya dini na hasa kwa kati ya dini zinazoamini katika Mungu mmoja.

Karidinali Walter Kasper aliendelea kueleza kwamba, leo kuna matumizi haya mabaya ya dini ambayo mara nyingi imekuwa kisingizio cha machafuko. Lakini ukweli wa machafuko hayo ni sababu au maslahi ya kiuchumi , kisiasa, kijamii. Na inapaswa kukumbukwa na wote kwamba, dini ni kwa ajili ya amani , amani ambalo ni jina la Mungu, na kwa hiyo dini anatuita katika kuwa na amani , kuthamini na kumtambua mtu mwingine,kuwa pia ameumbwa kwa mfano wa Mungu . Kusadiki hilo ni kuitakatifusha dini na fikira zinazo lenga katika kiini cha dini na moyo wa kubadilika , na kuwa na mtu wa amani , yaani kuishi na Mungu ndani ya moyo. Ni kuwa na amani ya kweli itokayo moyoni .

Na Abdelfatah Mourou , Makamu wa Rais wa chama cha Ennahdha Tunisia, na mwandishi wa Katiba mpya, amehoji iwapo vurugu na manyanyaso yamevaa mavazi ya dini nyenye kukiuka haki za binadamu, ambayo hakuna tena haki katika kiuchumi, heshima kwa haki za kijamii na kisiasa. Na iwapo jina la Mungu yaani amani linatumika katika maana yake halisi? Kwa swali hilo, alisema , Jibu ni lazima kila kiongozi wa dini ahubiri umuhimu wa kuachana na unyanyasaji na vurugu, kwa sababu hakuna dini inayofundisha udikteta, au mawazo ya kibaguzi, au ubinafsi kiuchumi , na masuala mengine yanayo sababisha shida za kijamii. Watu wanahitaji zaidi haki kutekelezwa . Kupotoshwa kwa nia za kidini na haki hasa na viongozi , ndiyo chanzo cha vurugu na manyanyaso yanayo jitokeza sasa.
Na Andrea Ricardi, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio amesema , hakuna dini inayo tetea vurugu, vurugu zinazo tokea ni majaribu makali dhidi ya dini,hivyo yanayohitaji uponyaji wa ndani ya roho.








All the contents on this site are copyrighted ©.