2014-02-20 12:18:44

Hotuba ya Papa kwa kikao Maalum cha Baraza la Makardinali Vatican


Makardinali wote wamekusanyika mjini Vatican kwa ajili ya kikao maalum cha Baraza la Makardinali kinachojulikana kama "Consistori", kilichoanza mapema asubuhi ya Alhamis hii mjini Vatican, ambamo Jumamosi ijayo, Makardinali wapya 19 waliotajwa na Papa hivi karibuni , watafanywa kuwa Makardnali..

Papa katika salaam zake kwa Makardinali, amewaomba Makardinali wote, kuzamisha mawazo yao katika umuhimu wa kuweka mbele uzuri wa familia na ukuu wa ndoa , kweli ya maisha ya binadamu, ambayo huonekana kuwa mepesi , lakini ndani mwake mmejaa utajiri mwingi wa furaha na matumaini, mapambano na mateso, kama sehemu ya maisha . Na kwamba, katika kikao hiki wanatafuta kuzama zaidi katika misingi ya kiteolojia juu ya familia na kutambua shughuli za kichungaji katika mahitaji ya mazingira ya wakati huu.

Papa ameeleza na kurejea historia ya binadamu kwamba, tangu mwanzo, Muumba alimbariki mwanamume na mwanamke ili wapate kuzaa, kuongezeka na hivyo hivyo kuwa na familia katika mfano wa Utatu wa Mungu duniani .

Papa amewataka Makardinali kutekeleza hayo lakini wakiwa makini na bila ya ugandamizaji, pia bila ya kupoteza onjo na ubora kazi zao za kichungaji. Leo hii Papa ameasa , familia inaonekana kupuuzwa na kunyanyaswa. Hivyo wao kama viongozi wa kanisa, wanatakiwa kukiri uzuri na ukweli na jinsi ilivyo vyema kuanza familia leo hii , na jinsi familia ilivyo ya lazima kwa maisha ya dunia na binadamu wa baadaye. Na kwamba, wameitwa kuufankisha mpango mkubwa wa Mungu kwa ajili ya familia na kusaidia wanandoa kuishi kwa furaha mpango huu katika maisha yao, na kuongozana na wanadoa katika matatizoyao mengi .

Papa alikamilisha hotuba yake kwa kumshukuru Kardinali Walter Kasper kwa mchango wake muhimu .








All the contents on this site are copyrighted ©.