Vishawishi vya majaribu huweza kuua, lakini Neno la Yesu huokoa.
(Vatican) Kushinda upotofu wa vishawishi vya majaribu inawezekana tu kwa kusikiliza
Neno la Yesu. Papa Francisko alieleza katika homilia yake wakati wa Ibada ya Misa
ya Jumanne asubuhi, aliyo iongoza katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican.
Alisema pamoja na udhaifu wetu , daima Kristo hutupatia imani na kufungua upeo wa
macho na uwezo, katika kuiona mipaka yetu.
Majaribu huonekana kama kivutio
poa ambacho taratibu humwingiza mtu dani ya ngome na kumfanya kuwa mtumwa na kiziwi
kwa neno la Mungu. Hotuba ya Papa Francisko ilieleza ukweli huo kufanya rejea mfululizo
wa maelezo ya Mtakatifu Yakobo, kama ilivyokuwa katika somo la Liturujia. Papa alieleza
Ukweli kwamba Mungu hamtengi binadamu yoyote, ila binadamu hujitenga mwenyewe kwa
nia na tamaa zake mbaya . Mtume Yakobo anasema, tamaa huzalisha dhambi. Na dhambi
huzalisha mauti.
Papa aliendelea kuuliza majaribu hutoka wapi ? Na kwa jinsi
gani hututendea ndani mwetu ? alisema ,maelezo ya Mtume Yakobo, yanatuambia kwamba,
majaribu hayatoki kwa Mungu , lakini hutokana na tamaa zetu, udhaifu wetu wa ndani,
ambao ni kovu la majeraha ya dhambi ya asili, ambalo likiendekezwa huzaa majaribu
kutokana na tamaa hizo. Na kwamba majaribu yana sifa tatu, ni kujiimarisha na
kujionyesha na kuvutia. Papa anasema, hujiimarisha na kutoa kishawishi kama ni haki.
Na hufanyika katika hali ya kuvutia na utulivu, kama Yesu mwenyewe alivyo eleza
katika mfano wa ngano na magugu. Ngano ina magugu yaliyopandwa na adui vilikua pamoja.
Hivyo majaribu hukua ama hakuna cha kuyazuia.
Papa aliendela kuasa kwamba,
hivyo , wakati wa majaribu, tunakatishwa hamu ya kuisikiliza sauti ya Mungu, tunakataa
kusikiliza neno lake. Tunazongwa na kushindwa tunakuwa hatuelewi. Na Yesu alikumbusha
wakati wa muujiza wa kuzidisha mikate, aliwaambia watoke nje ya mazingira ambayo
, yalikuwa yamefunga mioyo yao na upeo wa akili na macho yao na hivyo wakiongozwa
katika kutenda dhambi. Hivyo kusikiliza tu Neno la Mungu, Neno la Yesu la kuokoa.
Kusikia Neno la Mungu ni kufungua upeo wa macho ... Yeye daima hutufundisha jinsi
ya kuepuka majaribu. Yesu ni Mkuu , kwa sababu, si tu hutuwezesha kuyashinda majaribu
, lakini pia hutupatia uwezo a kujiamini zaidi katika kukataa vishawishi vya majaribu.
Imani hii , Papa anasema, ina nguvu kubwa. Na wakati wa kujaribiwa Bwana
anatarajia, imani yetu kuwa imara kuishinda dhambi. Daima ni kufungua upeo wa akili
na macho, kukataa kwa kuwa kinyume chake, mara kwa mara, ni kuelekea kuzimu. Majaribu
huja kama ilivyokuwa wakati wa mashua ya Mitume ilipopigwa na upepo. Kwenye mazingira
ya namna hii, alimalizia Papa , inawezekana tu kushinda majaribu kwa kusikiliza neno
la Yesu .
Hivyo , "Tunaomba kwa Bwana siku zote , kama walivyofanya Mitume,
na kwa uvumilivu wake , wakati sisi tunapambana na majaribu, Yeye awe karibu nasi
kutuhimiza tusikubali kushindwa au kuwa na wasiwasi,lakini tuyakumbuke mengi aliyo
tututendea kwa neema zake wakati ule. Bwana anasema, inua macho yako na utazame
upeo wa macho, si karibu, bali ni kusonga mbele. Ni hili Neno la kuokoa wakati wa
kuaguka katika dhambi na wakati wa majaribu".