2014-02-18 08:27:34

Baraza la Makardinali wanane wameanza kikao chao.


(Vatican Radio) Padre Federico Lombardi Jumatatu alikutana na waandishi wa habari kwa lengo la kuwapa muhtasari wa maelezo kuhusu mkutano wa Baraza la Makardinali na mikutano mingine muhimu ya Papa Francisko na washauri wake wa karibu, kama itakavyo jitokeza wiki hii.
Padre Lombardi amesema , wiki hii Baraza la Makardinali Wanane, akiwemo Katibu wa Nchi ya Vatican , Kardinali -mteule Pietro Parolin , watakuwa na kikao chao, kilichoanza Mapema Jumatatu kwa Ibada ya Misa , wakiwa na Papa, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la mjini Vatican, kabla ya kuingia katika chumba cha Kikao kilicho karibu na hapo.
Sehemu ya kwanza ya kikao ilikuwa ni kusikiliza ripoti kutoka Tume juu ya Shirika la kiuchumi na miundo mbinu ya utawala katika Jimbo la Papa , kazi iliyo wasilishwa na wajumbe watatu wa tume hiyo. Padre Lombardi alibainisha kuwa hakuna maamuzi yaliyofanywa na tume hiyo ambayo wajumbe wake ni walei wa kawaida, lakini walitoa taarifa ya kipindi cha miezi saba ya kwanza ya kazi zake, tangu ilipoundwa na Papa Francisko, Julai mwaka jana .

Jumanne Makardinali wanatarajiwa kupokea ripoti ya kutoka ya Tume ya pili Maalum iliyowekwa na Papa Francisko kusimamia utendaji wa masuala ya uchumi katika Taasisi ya Katoliki, ambayo inajulikana kama Benk ya Vatican .

Na Jumatano Papa Francisko na Wajumb e wa Baraza la Makardinali Wanane, watakutana na Makardinali wengine 15 ambao ni wajumbe wa Baraza la Makardinali la kwa ajili ya Masuala yanayohusiana na Uchumi na Fedha katika Jimbo la Papa.

Na Alhamisi asubuhi, itakuwa ni mwanzo wa siku mbili za Mkutano ulio nje ya ratiba ya mikutano ya Makardinali “ Consistory” , utakao fanyika katika Ukumbi mpya wa Sinodi,. Mkutnao huu utahudhuriwa na Makardinali wote kwa ajili ya kujadili Mada juu ya Familia. Baada ya Sala ya Masifu ya kati asubuhi, Decano wa Decania ya Makardinali , Kardinali Angelo Sodan, atafungua mkutano na Papa Francis anatarajiwa kusalimiana na Makardinali. Kardinali Walter Kasper , Rais wa zamani wa Baraza la Kipapa kwa Umoja wa Kikristo , kisha kutoa baadhi ya tafakari juu ya mada ambayo itajadiliwa na Makardinali wote wakati wa vikao vitakavyo fuatia.








All the contents on this site are copyrighted ©.