2014-02-17 11:25:26

Umoja wa Mataifa unaangalia uwezekano wa kuendeleza vikwazo vvya biashara ya silaha nchini Somalia


Taarifa ya wataalam wa mambo ya ulinzi na usalama kutoka Umoja wa Mataifa inaonesha kwamba, hali ya ulinzi na usalama bado ni tete nchini Somalia, jambo ambalo limeridhiwa na Serikali ya Somalia. Kutokana na ukweli huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linangalia uwezekano wa kuendelea kuiwekea vikwazo vya biashara ya silaha Somalia ilivyowekewa kunako Mwaka 1992 ili kuimarisha ulinzi na usalama.

Wachunguzi wa mambo wanasema, kuregezwa kwa vikwazo vya silaha nchini Somalia, kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa ni chanzo cha machafuko ya hali ya kisiasa na kijamii nchini Somalia. Wazo la kuendeleza vikwazo vya biashara ya silaha nchini Somalia lilikwisha tolewa na Mashirika ya Misaada ya Kimataifa pamoja na vyama vya kiraia, kwani biashara ya silaha ikiruhusiwa nchini Somalia, maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini kwani zinaweza kuangukia mikononi mwa watu vikosi vya waasi na vikundi vya kigaidi!







All the contents on this site are copyrighted ©.