Tunaendelea kujielimisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na maisha mchanganyiko,
tukiwa ndani ya familia ambamo kwa kawaida tuna baba , mama, watoto na wazee na wagonjwa.
Wanasayansi wanasema kuzeeka ni suala la maendeleo kimaisha. Wazee ni chemchemi ya
maisha ya familia , jumuiya na hata katika mipango ya kijamii na kiuchumi.
Katika
vipindi vya nyuma tumewazungumzia , Baba na mama kama wakuu wa familia kwamba, wana
wajibu muhimu wa kujua kila hali na maendeleo ya kila mwana familia, kimaisha
na kiroho pia. Na ni wajibu wa watoto kuheshimu mila na desturi za wazazi wao.
Leo,
tunawazungumzia wazee , tunaoishi nao katika familia hata nje ya familia, wao kama
watangulizi wetu katika maisha. Tunawaheshimu tena kwa ufahamu kwamba, kuishi kwao
miaka mingi wamepata uzoefu wa kutosha kimaisha na wameona mengi pia na hivyo wanakuwa
ni hazina kubwa kwa vizazi vipya.
Wanasayansi wanasema kuzeeka ni suala la
maendeleo kimaisha. Wazee ni chemchemi ya furaha na mafanikio ya maisha katika familia
, jumuiya na hata katika mipango ya kijamii na kiuchumi.
Kwa kujali umuhimu
wa kundi hili la watu wazee ambao ni vijana wa juzi , Umoja wa Mataifa uliitangaza
tarehe Moja Oktoba kuwa Siku ya Kimataifa ya Wazee.
Baraza la Kipapa kwa ajili
ya Walei katika waraka wake wa kichungajiwa 1 Oktoba 1998, juu ya heshima ya watu
wazee na utume wao katika kanisa, unaeleza kwamba, Maendeleo ya kisayansi, hasa maendeleo
katika uwanja wa tiba na dawa, umechangia kwa kiasi kubwa katika miongo ya hivi
karibuni, kuongeza muda wa wastani wa maisha ya binadamu. Uwepo wa kizazi cha tatu,
imekuwa sehemu kubwa ya idadi ya watu duniani : watu wastaafu katika kazi ya ajira
ya kazi, lakini, wanabaki kuwa rasilimali kubwa ndani ya familia , wakiwa na uwezo
wa kutoa mchango kwa manufaa ya familia na umma.
Kwa mujibu wa habari za
watu , watu wanaostahili kuwekwa katika kundi la kuitwa wazee ambao majuzi walikuwa
ni Vijana, ni watu walio katika umri wa miaka kati ya 65 hadi 75. Baada ya miaka
hiyo mtu anapata heshima zaidi ya kuitwa mkongwe.
Kanisa pamoja na kufurahia
mwendelezo wa wastani wa kuishi watu , pia linahofia kupungua kwa kiwango kikubwa
cha watu wanaozaliwa yaani watoto. Katika ukweli wake, ikilinganishwa na miaka ya
nyuma kwa wakati huu inakwenda kinyume kwamba idadi ya wazee inakuwa kubwa kuliko
idadi ya vijana na watoto ,kama inavyo onekana katika grafu ya idadi ya watu dunianiya
Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2002. Idadi ya wazee inazidi kuongezeka , wakati vijana
wanapungua. Mabadiliko haya yaliyoanza katika nchi za Kaskazini mwa Dunia kwa sasa
yana enea kwa kasi sana katika ulimwengu wa Kusini.
Nalo Shirika la Afya la
Dunia (WHO) katika taarifa yake ya March 28, 2012 ilidhihirisha kwamba, Idadi ya watu
duniani iko katika kasi ya kuzeeka, kwamba kati ya mwaka 2000 na 2050 , idadi ya watu
duniani walio na umri wa zaidi ya miaka 60 itakuwa mara mbili kutoka asilimia 11%
hadi 22%. Idadi kamili ya watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi linatarajiwa kuongezeka
kutoka millioni 605 millioni hadi billioni 2 katika kipindi hicho. Na kwamba nchi
za kipato cha kati zitaona mabadiliko haya kwa kasi zaidi.
Ripoti ya WHO inaendelea
kusema Dunia katika miongo michache ijayo itakuwa na watu zaidi wenye umri wa miaka
80 na 90 zaidi kuliko ilivyokuwa kabla. Kihistoria dunia haijawahi kushuhudia uwepo
wa watu wenye wengi umri wa kati na watu wazima, idadi iliyo zaidi ya watoto. Huu
ni uzoefu mpya, wazazi kuendelea kuwa hai, kama ilivyo leo, watoto kuwaona wazazi
wao, mababu na mabibi zao na hata Mabibi na Baba wakubwa.Kwa wastani, wanawake huishi
miaka sita hadi nane zaidi ya wanaume.
Na kwa jinsi gani , umri mkubwa unavyoweza
kuwa mzuri na wa manufaa, inategemea sababu nyingi, ikiwemo uwezo wa kazi wa mtu binafsi
katika mfumo wake wa kibiolojia , ikiwemo pia tabia na maambukizi katika maisha,
bila ya kusahau kile mtu anacho kula , anachofanya na uwezo wa kujikinga na hatari
za afya kama zile zinazo sababishwa na sigara, matumizi ya pombe, au sumu nyingine.
Taarifa pia inasema, kimataifa, watu wengi zaidi hufariki mapema kutokana
na huduma mbovu. Karibia 4-6% ya wazee katika nchi zilizoendelea wamesha kumbana
na matatizo ya kutendewa vibaya nyumbani .Hata katika taasisi wazee wengi hupambana
na kukemewa, kutukanwa , na hasa wenye wazee wagonjwa wasio jiweza kimwili, hunyima
hadhi ya utu wao (kwa mfano kwa kuwaacha katika nguo chafu, kunyimwa chakula, kutosikilizwa
haja na moni yao, kunyimwa haki ya kuchagua wnachopenda n,k ) . Tafiti juu ya mambo
ya wazee zinaonyesha kwamba, vitendo viovu dhidi ya wazee husababisha majeraha makubwa
ya kimwili na Kisaikolojia kwa muda mrefu .
Mama Kanisa kwa sasa anajali kwamba,
Idadi hii kubwa ya watu wazima kwa sasa, baada ya kupita miongo miwili mitatu, watakuwa
na uwezo mdogo wa kujihudumia kama tulivyoelezwa kwamba , katika nchi zinazoendelea,
inatabiriwa idadi ya wazee itaongezeka kwa mara nne zaidi ifikapo mwaka 2050. Kutakuwa
na wazee wengi na wakongwe, waliopoteza uwezo wao wa kuishi kwa kujitegemea wenyewe
kwa sababu mbalimbali kama uhamiaji, udhaifu kutokana na maradhi au matatizo mengine
ya kimwili au kiakili . Na hivyo wengi wao watakuwa wakihitaji huduma ya muda mrefu
kutoka kwa vijana, ambao nao idadi yao haitakidhi mahitaji ya wingi wa wazee wanaohitaji
kuhudumiwa. Upungufu huu wa vijana, unatokana na wazee hao kukataa kuzaa kwa makusudi
ya kukwepa usumbufu, ubinafsi na ubahiri.. Hata kama kutakuwa na nyumba za kuwaweka
wazee pamoja, bado makazi hayo yatahita kuhudumiwa na jamii ,kusaidiwa kimaisha.
Taarifa
inazidi kuogopesha kwamba, kuna hatari wazee wengi kupatwa na maradhi ya akili, hasa
kutokana na upweke, ikikadiriwa kuwa asilimia 25-30 % ya watu wenye umri wa miaka
85 au zaidi, watapatwa na maradhi ya akili hasa ugonjwa a kusahau na utambuzi . Mpaka
sasa wazee wenye shida hii ya akili hasa katika nchi za kipato cha kati na chini
, wengi wao hawapati huduma endelevu katika taasisi za kiserikali . Mara nyingi uzito
wa maatizo ya wazee, hubebwa na familia zao, huwafadhili na kuwahudumia nyumbani.
Ikiwa ndivyo, Je itakuwaje kwa wazima wa sasa wanaokata kuzaa watoto kwa makusudi,
wakati watakapofikia umri huo mkubwa ? Ina maafa watabaki peke yao majumbani bila
huduma, na pia hakuna mwendelezo wa kizazi. Hivyo unakuwa ni mwisho wa familia yake
katika uso wa dunia.
Na katika hali ya dharura, wazee huathirika zaidi , mfano
kunapotokea majanga asilia au vita, wazee na wakongwe hawawezi kukimbia haraka au
kusafiri umbali mrefu na hivyo huachwa nyuma wakiteseka, licha ya kuwa rasilimali
muhimu kwa jamii zao na pia kama chemchemi ya mawazo katika mchakato wa misaada ya
kibinadamu, katika ushiriki wao kama viongozi wa jamii
Kwa kujali upungufu
wa kizazi kipya, Kanisa linasema, hii ni changamoto kwa dunia, inayohitaji mapinduzi
ya haraka, vinginevyo ni kiama cha dunia. Dunia inapaswa kufanya mapinduzi ya katika
suala hili idadi ya vijana kuzidi kushuka, vinginevyo itasababisha matatizo ya kijamii
, kiuchumi, kiutamaduni , kisaikolojia na kiroho.
Katikati ya mwaka 1982, Dunia
ilifanya mkutano wa Kimataifa juu ya Wazee uhuko Vienna , Austria, mkutano uliobaki
kuwa rejea katika kumbukumbu za Kimataifa, juu ya wazee.
Katika makalamengine
yatayofuatia tutatazama matokeo ya majadiliano mbalimbali yaliyofanywa na Umoja wa
Mataifa, ambayo yametoa Kanuni mbalimbali juu ya kundi la watu wazee.