2014-02-15 15:21:19

Ombeeni amani Barani Afrika!


Vita, kinzani na migogoro inayoendelea kujitokeza Barani Afrika imekuwa ni chanzo kikubwa cha taabu na mahangaiko ya watu wasiokuwa na hatia. Kuna watu wanalazimika kuyakimbia makazi yao, wanateseka kwa njaa na magonjwa kutokana na ukosefu wa amani na utulivu.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuguswa na mahangaiko ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, anawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii, kumuunga mkono katika kusali kwa ajili ya kuombea amani na utulivu huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati na Sudan ya Kusini.







All the contents on this site are copyrighted ©.