2014-02-14 10:56:54

Papa Francisko kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Parokia ya Mtume Thoma, Jimbo kuu la Roma


Katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Parokia ya Mtakatifu Thoma Mtume ilipoanzishwa Jimbo kuu la Roma, Jumapili ijayo tarehe 16 Februari 2014, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kutembelea na kuadhimisha Fumbo la Ekaristi Takatifu majira ya jioni. Atapata fursa ya kutoa Sakramenti ya Upatanisho, kukutana na Halmashauri ya Walei Parokia pamoja na Familia ya Mungu katika ujumla wake.

Watoto waliobatizwa katika Kipindi cha Mwaka 2014 pamoja na wazazi wao, watabahtika kusalimiana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko, ili aweze kuwaimarisha katika imani yao kwa Kristo na Kanisa lake. Hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko inalena kuwaimarisha ndugu zake katika imani na maisha ya Kikristo na kwamba, kilele cha hija hii ni Adhimisho la Fumbo la Ekaristi Takatifu. Waamini wameanda zawadi maalum kama kielelezo cha mshikamano wao na Papa katika kusikiliza kilio cha maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.







All the contents on this site are copyrighted ©.