2014-02-13 12:12:09

Vatican na Israeli waridhia na hatua ya majadiliano iliyofikiwa hadi sasa!


Tume ya Kudumu ya ushirikiano kati ya Israeli na Vatican, hivi karibuni imehitimisha mkutano wake wa kawaida uliofanyika mjini Yerusalem kwa kujikita katika Kipengele cha 10ยง Ibara 2 inayohusu Makubaliano ya Msingi.

Mkutano huu umeratibiwa na Bwana Ze'ev Elkin, Naibu Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israeli pamoja na Askofu Antoine Camilleri, katibu mkuu msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Tume imejadili mambo msingi yaliyobakia katika Hati ya Jumla na kwamba, wote wameridhika na maendeleo yaliyokwishafikiwa kati ya Israeli na Vatican tangu walipohitimisha mkutano wao wa mwisho Juni, 2013. Mkutano utakaofuatia utafanyika mwezi Juni, 2014 hapa mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.