2014-02-10 12:11:18

Waombeeni Mapadre wenu waaminifu wanaojisadaka kwa ajili ya ndugu zao katika Kristo


Kuna kundi kubwa la Mapadre wema na watakatifu wanaoendelea kujitosa bila ya kujibakiza kwa ajili ya kuwahudumia watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia kiroho na kimwili. Hawa ni wahudumu wa Neno la Mungu, Sakramenti za Kanisa na Matendo ya huruma. Ni watu wanaojisadaka hata kwa gharama ya maisha yao wenyewe!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali na kuwaombea Mapadre wema na watakatifu wanaojisadaka kwa ajili ya ndugu zao katika Kristo kwa ukarimu, unyenyekevu bila hata ya kutafuta makuu!







All the contents on this site are copyrighted ©.