2014-02-07 09:53:28

Mshikamano wa kidugu kwa watu walioguswa na ajali ya moto mjini Buenos Aires, Argentina!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam na rambirambi kwa wale wote waliokumbwa na ajali ya moto iliyotokea siku ya Jumatano tarehe 5 Februari 2014, huko Buenos Aires nchini Argentina. Watu tisa wamepoteza maisha, wengine saba wamejeruhiwa na watu kadhaa walikuwa hawajulikani mahali walipo! Serikali ya Argentina imetangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake aliomwandikia Askofu mkuu Mario Aurelio wa Jimbo kuu la Buenos Aires anaonesha masikitiko yake makuu kwa maafa haya makubwa yaliyowapata wananchi wa Argentina. Anaendelea kuungana nao katika sala na sadaka yake, ili Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo, aweze kuwafariji wote waliofikwa kwa msiba huu.

Anawaalika wananchi wa Argentina kuonesha moyo, mshikamano na upendo wa kidugu kwa wote walioguswa na maafa haya, anawafariji wote na kuwapatia baraka zake za kitume!







All the contents on this site are copyrighted ©.