Kesi ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaanza kusikilizwa nchini Ufaransa, baada
ya miaka 20!
Baada ya kuyoyoma miaka ishirini tangu yaliyopotokea mauaji ya kimbari nchini Rwanda
kunako Mwaka 1994 na kusababisha watu 800, 000 kupoteza maisha, mapema juma hili,
kesi ya mauaji ya kimbari imeanza kusikilizwa mjini Paris, Ufaransa.
Kwa takribani
miaka ishirini uhusiano kati ya Rwanda na Ufaransa ulisuasua kwa kiasi kikubwa, lakini
kwa sasa inaonekana kana kwamba, historia inazidi kusonga mbele. Hayo yamesemwa na
Johnston Businge, Waziri wa sheria nchini Rwanda na kwa upande wake, Laurent Fabius
anasema ni vyema ikiwa kama kesi hii imepata mahali pa kusikilizwa.
Kwa miaka
kadhaa Serikali ya Rwanda ilikuwa inawadaia watuhumiwa wa mauaji ya kimbari waliokuwa
wamekimbilia nchini Ufaransa kurudishwa nchini Rwanda ili kujibu shutuma za mauaji
ya kimbari zilizokuwa zinawakabili, lakini kwa miaka hii yote Serikali ya Ufaransa
ilikataa kuridhia ombi la Serikali ya Rwanda.