2014-02-05 15:38:59

Wakatoliki ni muhimu kushiriki Ibada ya Misa na Ekaristi- Papa asema


Licha ya hali mbya ya hewa, baridi na mvua , waamini zaidi ya 25,000 walikusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kusikiliza mafundisho Papa , ambayo huyatoa kila asubuhi ya Jumatano akiwa Vatican. Kwa Jumatano hii ametoa mafundisho juu ya sakramenti ya Ekaristi , kiini cha imani ya Mkristu na chemichemi ya maisha ya Kanisa, ubatizo na kipaimara.
.
Papa amesema kutoka katika sakramenti hii ya upendo, katika kila muumini anapoipokea ka imani ya kweli, hutengeneza njia ya kutembea katika maisha yake halisi ya imani, ushirika na ushuhida. Ni jambo tunalo lishuhudia wakati tunakusanyika mbele ya Altare, wakati wa Ibada ya misa ya Ekaristi , tayari hutuonyesha sisi maana ya maisha ya mmoja kuwa karibu na mwingine, katika kugawana vipaji na mahitaji tunayojaliwa na kudra.

Papa aliendelea kutazama jinsi altare ilivyofunikwa kwa kitambaa cheupe , akisema kinatupatia picha kwamba tupo katika karamu. Juu ya meza kuna msalaba , unatuonyeswha kwamba Yesu alijitola sadaka hadi Msalabani. Sadaka inayotolewa juu ya madhabahu ni Kristu mwenyewe, ambaye anakuwa chakula chetu cha kiroho. Ili kuipokea neeema hii ya kuungana nae ni lazimakupita chini ya msalaba huo. Na chini ya Msalaba kuna ishara ya mkate na mvinyo. Na Karibu na hivyo, kuna mimbari, mahali ambapo Neno la Mungu hutangazwa. Hii inaonyesha kwamba, tumekusanyika kumsikiliza Bwana ambaye anazungumza katika maandiko, kwa hiyo pamoja na neno lake pia tunapokea chakula ambao ni mwli wa Kristu. .


Papa aliendelea kufafanua maana ya Ekaristi akisema neno ekaristi , maana yake katika lugha ya kiyunani ni kushukura . Na Dhabihu ya mkate na divai huiitwa Sakramenti ya Ekaristi , kwa sababu ni kumshikuru Baba wa Mbinguni aliye tupenda sana, hadi kumtoa mwanae kuwa kafara kwa ajili ya kutuokoa dhidi ya dhambi zetu. Kwa upendo wake tunawekwa huru dhidi ya dhambi
.

"Aliendelea kueleza kwamba, Ekaristi kwa ufupi inakuwa ni ishara ya Mungu na mwanadamu kukutana pamoja. Ni ishara ya uwepo wa Yesu Kristo, Mungu wa kweli na mtu wa kweli kati ya wale wanao mwamini. Hivyo maadhimisho ya Ekaristi ni zaidi ya kuiona kama sikukuu ya kumbukumbu ya Pasaka ya Yesu, fumbo la wokovu wetu. Kidhamiri ni zaidi ya kumbukumbu ili inakuwa ni kushiriki kaika fumbo la mateso , kifo na ufufuo wa Kristo.

Sakramenti ya Ekaristi ni kilele cha hatua ya wokovu wa Mungu, uliofanikishwa na Bwana Yesu , aliyejifanya kuwa kama mkate wa kuvunjwa kwa ajili yetu, kwa ajili ya kutubadilisha sisi sote. Kupitia uvumilivu wake wote na upendo wake, na kwa mateso na kifo na ufufuko wake , alitia upya mioyo yetu na maisha yetu , akituunganisha na wengine kwa upendo. Ni kwa sababu hii kwamba, tunapokusanyika wakati wa Sakramenti hii , tunaambiwa “pokea mwili wa Kristu”, hii ina maana kwamba katika nguvu za Roho Mtakatifu tumeshiriki katika Ibada ya Misa ya Ekaristi, tumeungana na Kristu , katika umoja wa kina pekee na kristu, akitufanya tupate onjo halisi la kuungana na Baba wa mbinguni katika furaha ya uwingu na watakatifu wote. Furaha kuu iliyoje kukutana na Mungu uso kwa uso.
Papa alikamilisha Katekesi yake na wito wa kutosahau kumshukuru Bwana kwa zawadi anayotupatia tunapokea Ukaristia. . Ni zawadi kubwa. Na kwa ajili hiyo inakuwa ni muhimu sana kushiriki katika Ibada za Misa ya Jumapili , ambayo si kusali tu lakini pia katika umuhimu wake wa kupokea Komunio, mkate ambao ni mwili wa Yesu Kristo, ambao , huokoa , hutusamehe , hutuunganisha Baba. Papa aalisema ni vyema kufanya hivyo.

Kila Jumapili ni Siku ya Bwana.Ni siku ya waamini kwenda katika Ibada ya Misa, kwa sababu ni siku ya kufufuka kwa Bwana wao. Papa aliendelea kueleza umuhimu wa Jumapili akisema ni kwa ajilli ya kuipokea Ekaristi inayotufanya kujisikia kuwa tu mali ya Kanisa, tu Taifa lmoja la Mungu na sehemu ya mwili wa Mungu, ambaye ni Yesu Kristo. Na kamwe hatuchoki kuupokea utajiri huu wa kanisa .

Papa alieleza na kusema anasali ili i kwamba, Sakramenti ya Ekaristi iweze kudumisha uhai wa kanisa na na uwepo wake katika jumuiya zetu ujenge upendo na mshikamano kama wana wa Mungu mmoja.

Papa pia alisema ni muhimu kwa watoto kuandaliwa vyema , kabla ya kupokea komunio ya kwanza , kukutana na Kristu mwenyewe , kwa sababu hatua hii ya kwanza ni muhumu sana katika kudumisha urafiki huu ulioanza kati ya mtoto na Yesu baada ya ubatizo na kwa baadaye Kipaimara.








All the contents on this site are copyrighted ©.