2014-02-05 10:03:35

Mkiwa karibu na Yesu, mioyo yenu itajaa furaha na tabasamu la kukata na shoka litaonekana midomoni mwenu!


Vijana ni jeuri ya Kanisa la Jamii katika ujumla wake. Mama Kanisa anaendelea kuwekeza katika majiundo makini kwa vijana sehemu mbali mbali za dunia, ili waweze kutambua dhamana na wajibu wao ndani ya Kanisa na Jamii kwa ujumla. Vijana wanaalikwa kutoka kifua mbele ili kuwatangazia watu Injili ya Furaha na kamwe wasiruhusu watu kuwapokonya matumaini yao kwa Kristo na Kanisa lake.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawaambia kwamba, Yesu anawakirimia zawadi ya maisha katika ukamilifu wake wote. Vijana wakijitahidi kuwa karibu na Yesu, kwa hakika watapata furaha katika mioyo yao pamoja na kuonesha tabasamu la kata na shoka midomoni mwao!







All the contents on this site are copyrighted ©.