2014-02-05 14:53:29

Askofu mkuu Santo Gangemi ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Mali


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Santo Gangemi, kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Mali na ataendelea pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Guinea. Hiki ni kielelezo cha mshikamano wa dhati kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa watu wanaoendelea kuteseka kutokana na majanga mbali mbali ya maisha Barani Afrika.

Baba Mtakatifu anaendelea kuhimiza majadiliano katika ukweli, uwazi na udugu kama njia ya kupambana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kujitokeza katika maisha ya watu sehemu mbali mbali za dunia, hususan migogoro ya kivita na kinzani za kijamii kama ilivyo nchini Mali.







All the contents on this site are copyrighted ©.