2014-02-04 15:49:13

Ujumbe wa Papa kwa Kwaresima, wadai majitoleo zaidi kwa wahitaji.


Jumanne hii , Ofisi ya habari ya Vatican imetoa Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya kipindi cha Kwaresima, kinachoanza tarehe 5 Marchi kwa ibada ya Majivu. Ujumbe huo, unaoongozwa na Madambiu: "Alijifanya Maskini kwa ajili Yenu , ili kutokana na umasikini wake awatajirishe”.

Papa, katika ujumbe huu, anawaelekeza wanakanisa kuyatazama kwa kina mahangaiko ya watu, katika hali zote, kibinadamu na kiroho pia, akilenga hasa kutoa msaada kimawazo , jinsi ya kuitembea njia ya uongofu kama mtu binafsi au kama jumuiya ya kanisa , kwa kuvuviwa na maneno ya Mtume Paulo “ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, lakini kwa ajili yenu, alijifanya maskini , ili kwa umaskini wake, uwatajirishe " (2 Kor 8:09 ).
Mtume Paulo aliwaandikia Wakristo wa Korintho, kwa nia ya kuwahamasisha watende kwa upendo na majitoleo zaidi ya wema na ukarimu, kwa ajili ya kusaidia waamini wa Jerusalemu waliokuwa katika mahitaji.

Baba Mtakatifu Francisko amehoji maneno hayo ya Mtume Paulo yana maana gani kwetu kama Wakristo wa leo? Mwaliko huu wa kuwa umaskini katika maisha ya kiinjili,una maanisha nini leo hii?

Baba Mtakatifu Francisko anasema katika ujumbe wake, zaidi ya yote inatuonyesha jinsi Mungu anavyofanya kazi yake. . kwamba yeye haonekani kupitia wenye nguvu na mamlaka ya kidunia au utajiri wa vitu, lakini kupitia watu wanyonge na dhaifu, watu maskini wasiokuwa na kitu: "ingawa alikuwa tajiri, lakini kwa ajili yenu , alijifanya maskini ...". Kristo, Mwana wa Mungu wa milele , aliye katika umoja na Baba wa mbinguni na katika nguvu na utukufu wake, , alichagua kuwa maskini,na kuja kukaa kati yetu na aliye karibu na kila mmoja wetu , alijifanya kuwa hana utukufu ili aweze kuwa kama sisi katika mambo yote (taz. Flp 2:07 ; Ebr 4:15).

Papa anaendeela kueleza kwamba, Mungu kujifanya mtu wa kawaida, hili ni tendo kubwa la kustajaabisha! Ni upendo unaojionyesha katika neema ya ukarimu,na hamu ya kuwa karibu na kushirikishana na wengine. Ni upendo wa kujitoa sadaka bila kusita kwa ajili ya wapendwa wengine. Ni kuwa mtu mwema mwenye huruma, aliye tayari kushirikiana na wengine kwa upendo katika mambo yote. Upendo unaotufanya kuwa sawa , Upendo unao tufanya sisi wote kufanana , upendo unaojenga usawa , na kuvunja kuta zote za utengano na zenye kutuweka mbali na wengine. Ni ndivyo Yesu, alivyoungana na binadamu katika kazi zake , kupitia wazo na akili ya kibinadamu , alitenda kwa maamuzi ya upendo ,na kwa moyo wa ubinadamu. Alikubali kuzaliwa na Bikira Maria , ili awe kweli mmoja wetu, katika mambo yote, ingawa yeye hakuwa na dhambi. " ( Gaudium et Spes , 22).


Papa ameendelea kutafakari kwamba, kwa kujifanya mwenyewe maskini , Yesu hakufanya hivyo kwa manufaa au faida yake mwenyewe lakini kwa ajili yetu, kama Mtakatifu Paulo anasema " kwamba umaskini wake ulituwezesha kuwa matajiri" . Maneno haya si kama ni mzaha au matani, bali yanaonyesha kwa ujumla, mantiki Mungu, mantiki ya upendo, mantiki ya mwili na msalaba. Mungu hakuudodosha wokovu wetu toka mbinguni hadi kwetu, lakini ulishusha kwetu kupitia mwanae aliyemwilisha na kujitoa sadaka, kwa hali ya ubinadamu na huruma. Upendo huu wa Kristo, kwa hakika ni wa kipekee. Yesu alijishusha katika ubinadamu hadi kuingia katika maji ya mto Jordan na kubatizwa na Yohane Mbatizaji alifanya hivyo si kwa sababu alihitaji kuongoka na kutubu dhambi lakini alifanya hivyo ili awe kati ya watu wake, waliohitaji kuongoka na kusamehewa dhambi zao, na Yeye akachukua msalaba wa dhambi zetu sisi . Kwa njia hii alichagua kutufariji , kutokoa na kutuweka huru dhidi ya taabu zetu.

Papa anasema pia kwamba, inashangaza kwamba Mtume Paulo anasema, kwamba tuliwekwa huru, si kwa utajiri wa Kristo lakini kwa umaskini wake . Mtume Paulo alieleza hilo , licha ya ufahamu wake juu ya " utajiri wake Kristo usiopimika " (Efe 3:08 ), na kwamba yeye ni " mrithi wa vitu vyote " (Ebr 1:02 ).

Ujumbe wa Papa pia umetaja mahangaiko na taabu za kimaadili , zinazotia wasiwasi, akitaja ni familia gapi leo hii ziko katika mateso na mahangaiko ambayo mara nyingi yanatokana na kuvunjika kwa ndoa, au vijana kujiingiza katika vitendo vilivyo nje ya uadilifu kama ulevi wa madawa na pombe wa kupindukia? Ni maumivu kwa familia kwa kuwa baadhi ya wanafamilia wako nje ya misingi ya haki za kijamii. Na kwamba wakati mwingine ukosefu wa haki ya ajira huwalazimisha kuingia katika taabu hii inayo wakosesha au kuwanyiima heshima ya kupata mkate wa kupeleka kuleta nyumbani. Papa ameendelea kutaja ukosefu wa usawa na heshima kwa haki za elimu na afya .

Kwa mitazamo hiyo Papa ameandika jinsi mahangaiko ya kimaadili , yanaweza kuwa chanjo kikuu cha watu kujiua.Taabu zinazomfunga mtu kimaadili mara huandamana na utomvu kiroho. Papa Francisko anasisita katika hili wakristu wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuitangaza Injili yenye kumweka mru huru dhidi ya minyororo hiyo. Amesema, ni kuuleleka ujumbe wa Injili katika mazingira hayo, kwamba Mungu ni msamehevu na anatupenda sote licha ya dhambi zetu. Na huduma yake ni ya bure, kwa ajili ya ushirika na uzima wa milele. "

Ujumbe wa Papa , unatoa mwaliko kwa watu wote, wake kwa waume ili kwamba, katika kipindi hiki cha Kwaresima, Kanisa zima liwe tayari kushuhudia ujumbe wa injili, hasa kwa wale wote ambao wanaishi katika ulimwengu wa vitu, uhaba wa maadili na ufukara wa kiroho, waweze kuuona utajiri wa kiinjili uliogubikwa ndani ya upendo na huruma ya Mungu Baba yetu, aliye tayari kukutana na kila mtu katika Kristo. Na Wakristu wanaweza kushuhudia hilo kwa kuyaishi maisha ya Kristu wenyewe aliyejifanya kuwa maskini kwa ajili ya kututajirisha sisi kwa umaskini wake.

Kipindi cha Kwaresima iwe ni kipindi cha kuiinua mioyo kwa Mungu kupitia njia za kujikatalia ; na kuwa wakarimu zaidi. Amemtaka kila mmoja kujiuliza mwenyewe, nini hasa anachotakiwa kujinyima , kwa ajili ya ajili ya kuwatajirisha wengine kupitia umaskini wake katika hilo alilojinyima. Na kwamba kujinyima kwa kweli , au maskini wa kweli huumiza. Na hakuna kujinyima kwa ukweli kusikoleta uchungu, na toba. Papa anaamini kwamba majitoleo yoyote yale yasiyoumiza roho si majitoleo ya kweli.

Papa anamwomba Roho Mtakatifu , ambaye kupitia kwake yeye pia alikuwa maskini kama sisi , aweze kuwatajirisha wote wanaojinyima kwa ajili ya kuwtajirisha wengine. Anasema kwa upande mmoja ni kutokuwa na kitu na kwa upande mwingine kumbe ni kutajirisha na kila jambo (2 Kor 6:10). Papa anasali ili waamini waendeleee kudumu katika maazimio yao n a ili waongezewe moyo wa kujali na kuwajibika kwa ajili ya umaskini wa watu wengine, na ili waweze kuwa na huruma na kutenda mema na fadhira zaidi .

Kwa ajili ya kuonyesha tumaini hili, Papa anaendelea kuweleza kwamba, anasali ili kwamba, kila muumini binafsi , na kama jumuiya ya Kanisa, iweze kutoa matunda mazuri katika kipindi hiki cha Kwaresima . Papa anasali kwa kila mmoja na ametoa pia wito kwa waamini amwombee. . Bwana awabariki na kuwaombea pia ulinzi wa Mama Maria.







All the contents on this site are copyrighted ©.