2014-02-03 14:03:50

Rais Tui Atua Tamasese Efi akutana na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatatu, tarehe 3 Februari 2014 amekutana na kuzungumza na Rais Tui Atua Tupua Tamasese Efi wa Visiwa vya Samoa, ambaye baadaye alikutana na kuzungumza na Askofu mkuu Pitero Parolin, katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo ya viongozi hawa wawili, wamejikita katika hali ya uchumi na kisiasa pamoja na kuangalia mchango wa Kanisa Katoliki katika mchakato wa maendeleo na ustawi wa wananchi wa Samoa katika medani mbali mbali za maisha. Wamebadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa hasa umuhimu wa ushirikiano wa Kikanda, utunzaji bora wa mazingira katika nchi zilizoko kwenye Bahari ya Pacific.







All the contents on this site are copyrighted ©.