2014-02-03 08:57:41

Mshikamano wa kidugu na watu waliokumbwa na mafuriko nchini Italia!


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuadhimisha Siku kuu ya kutolewa Bwana Hekaluni sanjari na Maadhimisho ya Siku ya 18 ya Watawa Duniani, Jumapili tarehe 2 Januari 2014, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, aliyaelekeza mawazo yake kwa wananchi wengi wa Italia ambao kwa wakati huu wamekumbwa na mafuriko ambayo tayari yamekwisha sababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao!

Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema, kuonesha moyo wa upendo na mshikamano kwa watu walioathirika kwa mafuriko haya. Kwa upande wake, ataendelea kuwa karibu nao kwa njia ya sala na sadaka yake.







All the contents on this site are copyrighted ©.